Baadhi ya wakurugenzi na viongozi wa Friedkin Conservation Fund wakiwa katika maonesho ya nanenane mwaka huu mkoani Simiyu
Mwandishi wetu,Arusha.
Taasisi
ya uhifadhi ya Friedkin Conservation Fund(FCF), imetoa msaada wa zaidi
ya sh 84 milioni kusaidia utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa jamii
ambayo inazunguka mapori ya akiba ya Moyowosi, Uvinza na Ugalla ili
kujikwamua na umasikini.
Meneja
Maendeleo ya jamii wa taasisi ya FCF yenye makao makuu jijini Arusha,
Nana Grosse-Woodley alisema fedha hizo ni sehemu ya misaada ya kijamii
ambayo imetolewa kati ya mwaka jana na mwaka huu katika eneo hilo ambapo
taasisi hiyo, kupitia kampuni yake kitalii ya Wengert Windrose Safaris iliyowekeza katika eneo hilo.
Grosse-Woodley
alisema fedha,zimetolewa katika kusaidia vikundi vya
ujasiriamali(VICOBA), kusaidia utengenezaji wa madawati
260,kuwatengenezea mizinga ya nyuki 130 wananchi na kugharamia kambi za
matibabu kwa wananchi wa eneo hilo.
"misaada
hii imekuwa na manufaa makubwa kwa jamii, kwani sasa baadhi wameweza
kuanzisha miradi yao, wengine kupona maradhi na katika shule tumesaidia
kupunguza tatizo la watoto kukaa chini kwa kukosa madawati"alisema.
Afisa
Maendeleo ya jamii ya FCF katika pori la akiba la Moyowosi na Uvinza.
Batro Ngilangwa alisema kampuni ya Wingert Windrose Safaris ambayo ipo
chini ya FCF, mwaka 2017 ilitumia kiasi cha sh 17.1milioni,katika
kusaidia miradi ya jamii.
Alisema
katika eneo la pori la Myowosi vikundi vya vikoba viliwezesha kiasi cha
sh 2.6 milioni, Wanafunzi walisaidia kulipiwa ada kiasi cha sh 1.5
milion na pia kiasi cha sh 1.7 kilitumika kukarabati darasa shule ya
msingi Migezi.
"katika
eneo la Uvinza mwaka 2017,FCF ilisaidia kulipia ada wanafunzi kiasi
cha sh 1.2 milioni,ujenzi kiwanja cha michezo 1.8 milion na vikundi vya
ufugaji wa nyuki vimenufaika na kiasi cha sh 9.9 milioni"alisema
Alisema
katika eneo la pori la akiba la Ugalla Kusini na Kaskazini mwaka 2017
kiasi cha sh 23.5 milioni zilitolewa kuchangia miradi ya
maendeleo.ikiwepo vikundi vya vikoba,ujenzi wa madarasa,ujenzi wa miradi
ya uvunaji maji ya mvua na udhamini wa wanafunzi.
Mapori
hayo ya Akiba ambayo yapo chini ya Usimamizi wa Mamlaka ya wanyamapori
nchini(TAWA), pia kumeweza kutokomezwa matukio ya ujangili kutokana na
ushirikiano mkubwa wa ulinzi baina ya askari wa TAWA, FCF na wananchi.
Post a Comment