Meneja wa masoko na mauzo wa Kampuni ya SBC(T) Lalit Sharma, akimkabidhi
mipira Katibu wa chama cha waandishi wa habari za michezo na burudani
mkoa wa Arusha, Mussa Juma kwa ajili ya Tamasha la kumi la waandishi wa
habari mkoa wa Arusha,Manyara na Dar es Salaam na wadau wa habari,
ambalo litafanyika Agoust 29 uwanja wa Sheikh Amri Abeid
Akizungumza
na waandishi wa habari, Palace Hotel , Katibu wa chama cha waandishi wa
habari za michezo mkoa wa Arusha(TASWA-Arusha), Mussa Juma, alisema
tayari maandalizi muhimu yamekamilika.
Juma
alisema Tamasha hilo linaloandaliwa na TASWA na kampuni ya Arusha
Media.mdhamini Mkuu ni Kampuni ya Bia nchini( TBL) kwa miaka 10 sasa,
litashirikisha michezo ya Soka, Mpira wa pete, kuvuta kamba na kukimbiza
kuku.
"tunapenda
kutangaza rasmi tamasha la 10 ya TASWA Arusha litafanyika Agosti 29 na
kauli mbiu yetu ni Uchaguzi Mkuu bila vurugu inawezekana"alisema
Alisema
katika Tamasha hilo, ambalo litashirikisha pia timu za wafanyakazi wa
kampuni ya bia nchini(TBL) Taasisi na Faidika na kampuni ya Pepsi
litaandamana na ziara ya wanahabari kutembelea Hifadhi ya Taifa ya
Arusha.
Nahodha wa timu ya TASWA Arusha, Ramadhani
Siwayombe akikabidhiwa jezi kwa ajili ya tamasha la waandishi wa habari
na wadau wa habari mkoa wa Arusha ambalo litafanyika Augosti 29 Sheikh
Amri Abeid, anayemkabidhi ni Filbert Masele meneja mikopo ya wafanyakazi
wa FAIDIKA na Meneja wa FAIDIKA mkoa wa Arusha Eliya Mlay hafla hiyo,
ilifanyika Palace hotel
Wakizungumza
katika kikao hicho, Meneja wa Masoko wa kampuni ya Mega Trade Edmund
Rutaraka, Meneja masoko wa kampuni ya SBC(T) Lalit Sharma na Meneja wa
Faidika Arusha,Eliya Mlay walisema wamedhamini Tamasha hilo ili
kuendeleza michezo.
Rutaraka alisema kampuni yao kwa miaka mitano sasa inadhamini tamasha hilo na wanajivunia mafanikio makubwa.
Tamasha
hilo, limedhaminiwa na kampuni ya bia nchini(TBL) Kampuni ya Mega
Trade,Shirika la hifadhi za Taifa(TANAPA),Shirika la Nyumba nchini (NHC)
Kampuni ya SBC(T) Ltd,Mamlaka hifadhi Ngorongoro(NCAA), Taasisi ya
FAIDIKA na Tanzanite One.
Makamu
Mwenyekiti wa TASWA Arusha, Andrea Ngobole alisema wadhamini wengine wa
Tamasha hilo watatangazwa ijumaa ya tarehe 22 august saa kumi jioni hapohapo hotel ya palace sambamba na zawadi na mgeni rasmi.
Meneja
wa masoko na mauzo wa Kampuni ya SBC(T) Lalit Sharma, akimkabidhi
mipira Katibu wa chama cha waandishi wa habari za michezo na burudani
mkoa wa Arusha, Mussa Juma kwa ajili ya Tamasha la kumi la waandishi wa
habari mkoa wa Arusha,Manyara na Dar es Salaam na wadau wa habari,
ambalo litafanyika Agoust 29 uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Makamu
Mwenyekiti wa TASWA mkoa wa Arusha,Andrea Ngobole, akipokea vikombe
kutoka kwa Filbert Masele meneja mikopo ya wafanyakazi wa FAIDIKA na
Meneja wa FAIDIKA mkoa wa Arusha Eliya Mlay jana Palace Hotel kwa ajili
ya tamasha la waandishi wa habari na ambalo litashirikisha pia
wafanyakazi wa taasisi hiyo, ambalo litafanyika Augost 29 uwanja wa Sheikh Amri Abeid
Wadhamini
na viongozi wa TASWA Arusha, wakiwa kwenye kikao na waandishi wa habari
kuelezea Bonanza la vyombo vya habari na wadau wa habari mkoa wa
Arusha,ambalo litafanyika Augosti 29 uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
|
Home
»
KITAIFA
»
Matukio
»
michezo
» TAMASHA LA KUMI LA MICHEZO LA WAANDISHI WA HABARI ARUSHA KUTIMUA VUMBI AGOSTI 29 SHEIKH AMRI ABEID STADIUM
About Author
Journalist , Enterpreneur, Lecturer and Blogger. Email :ngoboleaa@gmail.com.
Advertisement
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment