HABARI ZA MOROGORO: Mvua za leta tena maafa Morogoro! A+ A- Print Email PRINCE MEDIA TZ Link Author Title: HABARI ZA MOROGORO: Mvua za leta tena maafa Morogoro! Author: PRINCE MEDIA TZ Rating 5 of 5 Des: MVUA kubwa iliyoambatana na Upepo mkali, imeezua na kuangusha baadhi ya Mahema ya muda yanayotumiwa na Waathirika wa Mafuriko ya... MVUA kubwa iliyoambatana na Upepo mkali, imeezua na kuangusha baadhi ya Mahema ya muda yanayotumiwa na Waathirika wa Mafuriko yaliyotokea katika eneo la Matepeni na Magole Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro. Mvua hiyo iliyonyesha juma lililopita, mwaka huu, imeezua mahema 200 kati ya mahema 400, yaliyojengwa na Chama Cha Msalaba Mwekundu Tanzania, kwa ajili ya kusaidia wakazi zaidi ya 900 wa eneo hilo. Hata hivyo Wakazi hao, waliokubwa na mafuriko ambayo iliyotokea Januari 22, mwaka huu, bado wanaishi kwenye eneo ambalo limetengewa na Serikali kutokana na adha iliyowapata huku wakiendelea kusubiri hatima ya kupata misaada Zaidi kutoka Serikalini. Kufuatia hali hiyo, Chama Cha Msalaba Mwekundu, kimesema kitajenga upya Mahema hayo ili kuhakikisha waathirika hao wanapata hifadhi. Mwenyekitiwa Chama hicho hapa Nchini, Dr. George Nangale, amesema kuwa Chama hichokitatekeleza wajibu wake na kuhakikisha familia zote zinapata Makazi ya muda ambapoamewaomba wadau wengine waweze kujitokeza na kusaidia Wananchi hao.
Post a Comment