Mgeni rasmi akikabidhi zawadi wa jezi kwa mabingwa wa chemchem cup 2018 timu ya Manyara fc |
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti akikagua timu ya Manyara fc kabla ya mchezo kuanza |
Baadhi ya mashabiki wakishuhudia fainali ya mchezo huo |
Mkuu wa mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti akikabidhi kikombe kwa washindi wa miochuano hiyo timu ya manyara fc mara baada ya kuibukana ushindi wa goli mbili kwa bila |
Mfungaji bora wa mashindano hayo akibebwa na kushangiliwa kwa furaha na mashabiki wa Manyara fc |
Mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa Manyara Mnyeti akikabidhi zawadi ya jezi kwa washindi wa pili wa michuono hiyo ambao pia wamejipatia kitita cha shilingi milioni 1.1 |
Mkuu wa mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti akikagua timu zilizoingia fainalilya michuano ya chemchem cup 2018 |
Mwandishi wetu,Manyara
Timu ya soka ya Manyara FC imetwaa ubingwa wa michuano ya kupiga vita
ujangili ya Chemchem 2018, baada ya kuichapa timu ya majita FC magoli
2-1 katika mchezo wa fainali uliofanyika uwanja wa Chemchem, kijiji cha
Mdori wilayani Babati,mkoa wa Manyara.
Katika
mchezo huo ambao mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa mkoa Manyara, Alexander
Mnyeti magoli yote ya Manyara yalifungwa na Laurence Michael Dk ya3 na
87 huku goLi pekee la Majita likifungwa na Hassan Hamza dk ya 90.
Kutokana
na ushindi huo, Manyara FC walikabidhiwa zawadi ya fedha taslimu kiasi
cha sh 1.7 milioni, kikombe chenye thamani ya sh 500,000 na mpira na
seti ya jezi.huku Majita wakikabidhiwa fedha taslim 1.1 milioni, seti za
jezi na mpira.
Kabla
ya mchezo huo wa fainali, waliokuwa mabingwa watetezi, Mdori FC
walifanikiwa kushika nafasi ya tatu baada ya kuifunga kwa penati 4-3
timu ya Kalmaji baada ya kushindwa kupata mbabe dakika 90 na kuvuta sh
700,000 na setiya jezi huku Kalmaji wakipata 300,000.
Akizungumza
wakati akitoa zawadi, Mnyeti alipongeza taasisi ya Chemchem iliyowekeza
hoteli za kitalii katika eneo hilo la hifadhi ya jamii ya wanyamapori
ya burunge kwa kuanzisha ligi hiyo tangu mwaka 2014.
Alisema
michezo hiyo, imekuwa na faida kwani imehamasisha vita dhidi ya
ujangili, utunzwaji wa mazingira lakini pia imeibua vipaji vya vijana na
kujenga afya zao.
"kutokana
na mafanikio makubwa ya ligi hii ya Chemchem sasa nataka kuanza ligi ya
mkoa wa Manyara na kamati hii ya chem chem itasimamia kwa kushirikiana
na chama cha soka mkoa Manyara"alisema
Mkurugenzi
wa Chemchem Foundation, Riccardo Tossi,alisema michuano hiyo ambayo
imeshirikisha vijiji zaidi ya 10 vinavyozunguka burunge WMA, ambayo
inapakana na hifadhi za taifa za Tarangire na Manyara.
"michuano
hii imetumia zaidi ya sh 35 milioni na imefanikiwa sana kurejesha
mahusiano mazuri baina yetu na wananchi lakini pia kusaidia vita dhidi
ya ujangili.
Katibu
wa mashindano hayo, John Bura alisema jumla ya timu 20 za soka
zilishiriki na timu tatu za wanawake, ambapo timu zote zilipewa seti za
jezi na mipira.
Post a Comment