PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: MAIPAC,CANADA KUSHIRIKIANA KUSAIDIA WANAHABARI NA JAMII ZA PEMBEZONI
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
  Afisa miradi wa MAIPAC, Deborah Makando akimvisha crown Lori Legault katika hafla fupi ya kumuaga mtaalamu huyu aliyerejea kwao mara baada...

 

Afisa miradi wa MAIPAC, Deborah Makando akimvisha crown Lori Legault katika hafla fupi ya kumuaga mtaalamu huyu aliyerejea kwao mara baada ya kukamilisha mafunzo ya wiki mbili

Mtaalamu wa masuala ya andiko la miradi toka Canada Lori Legault akiwa na furaha baada ya kukamilisha wiki mbili za mafunzo aliyotoa kwa waafanyakazi wa MAIPAC 

Mkurugenzi wa MAIPAC Musa Juma kulia akimkambidhi cheti cha shukrani mshauri elekezi Lori Legault toka Canada baada ya kumaliza mafunzo ya kuwajengea uwezo timu ya MAIPAC kwa muda wa wiki mbili.
 


Mwandishi wetu. Arusha.

Taasisi ya Wanahabari wa kusaidia jamii za Pembezoni (MAIPAC) inatarajiwa kuwa na mashirikiano na taasisi zisizo za kiserikali za nchini CANADA ili kuwajengea uwezo wanahabari na kusaidia jamii ya Pembezoni.

Mkurugenzi wa shirika la MAIPAC, Mussa Juma alitoa taarifa jana katika hafla ya kumuaga mshauri elekezi wa MAIPAC kutoka nchini Canada, Lori Legault ambaye alikuwa nchini kulijengea uwezo shirika la MAIPAC.

Juma amesema licha ya mshauri huyo kutoa mafunzo kwa MAIPAC jinsi ya kuandaa miradi na kutafuta wafadhili walifikia makubaliano ya kuwa na mahusiano na mashirika ya Canada ambayo yanajihusisha na kusaidia jamii za pembezoni na wanahabari.

Amesema mtaalam huyo ambaye ameletwa nchini maalum kusaidia MAIPAC na taasisi ya CESO  kwa ushirikiano na ubalozi wa Canada, ujio wake umekuwa na mafanikio makubwa.

Awali Legault alisema  anashukuru kuja nchini Tanzania na kufanyakazi na MAIPAC kwani pia amejifunza utekelezwaji miradi  ya MAIPAC .

Amesema amejionea kazi za mradi wa uhifadhi mazingira,Vyanzo vya maji na Misitu  kwa maarifa asilia ambao unafadhiliwa na shirika la Maendeleo la umoja wa Mataifa(UNDP) na kusimamiwa na jumuiko la maliasili Tanzania(TNRF).

"Nimefurahi kuwa Tanzania na MAIPAC watu wa Tanzania ni wakarimu sana na tutaendelea kushirikiana"alisema

Afisa miradi wa Maipac, Deborah Makando akipewa maelekezo na Lori Legault ya namna bora ya kuandika na kusimamia utekelezaji wa miradi 

Afisa Miradi wa MAIPAC, Debora Makando alisema wamejifunza mengi kutoka kwa mfadhili huyo.

Makando alisema kutokana na mafunzo waliyopata wataboresha utendaji wa kazi wa MAIPAC.

Afisa Tawala wa MAIPAC Andrea Ngobole alisema wanahabari na jamii za pembezoni zitanufaika na mahusiano ya MAIPAC na Taasisi za Canada na CESO.

"tunataraji kuwa na miradi ya kubadilishana uzoefu kusaidia jamii za pembezo na athari za mabadiliko ya tabia nchi.

MAIPAC Team wakiwa katika picha ya pamoja na Bi. Lori Legault mara baada ya kuwa na hafla fupi ya kumuaga mtaalam huyo.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top