Wananchi mbalimbali wakipata maelezo na umuhimu wa utalii ndani ya mabanda ya utalii katika maonesho ya nanenane Mkoani Simiyu yanakofanyika kitaifa mkoani hapa |
Mabanda ya taasisi za uhifadhi za Shirika la hifadhi za Taifa(TANAPA),taasisi ya uhifadhi ya Friedkin Conservation Fund(FCF) na Ngorongoro yamekuwa vivutio vya wananchi wanaoshiriki Maonesho ya wakulima na wafugaji nane nane mwaka huu kitaifa mkoani Simiyu.
Taasisi
za uhifadhi hizo ,Shirika la hifadhi za Taifa(TANAPA),Friedkin
conservation Fund (FCF) na Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro,wamekuwa
wakitoa elimu ya uhifadhi ,vita dhidi ya ujangili na kuna ofa za
kutembelea uhifadhi katika hifadhi za Taifa na mamlaka ya hifadhi Ngorongoro.
Meneja
kitengo cha ujirani Mwema cha shirika la hifadhi za Taifa(TANAPA),Ahmed
Mbugi alisema shirika hilo limejipanga kutumia maonesho haya kutangaza
utalii.
Mbugi alisema
katika maonesho hayo,TANAPA itatoa magari kuwapeleka watalii hifadhi za
taifa za Serengeti kwa washiriki wa maonesho ya kitaifa mkoani Simiyu.
Alisema kwa wanaoshiriki maonesho mkoa wa Morogoro watapelekwa Hifadhi ya Taifa ya mikumi kwa kuchangia gharama.
Katika
maonesho hayo,pia Taasisi binafsi za uhifadhi zitatoa huduma ikiwepo
taasisi ya Friedkin conservation Fund(FCF) ambayo kwa mara ya kwanza
itashiriki mwaka huu.
Meneja
uhusiano wa Friedkin Conservation Clarence Msafiri alisema katika
maonesho ya mwaka huu wanatoa elimu ya uhifadhi na vita dhidi ya
ujangili.
"Pia
tutahamasisha watanzania kwenda kutembelea vivutio vya utalii katika
mapori ya akiba ambayo tumewekeza ikiwepo eneo la makao kwa wakazi wa
kanda ya ziwa" alisema
Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro(NCAA) pia wanatumia maonesho hayo kupeleka watalii wa ndani ya mamlaka ya hifadhi kuona vivutio vilivyopo Ngorongoro.
Naibu
Mhifadhi Mkuu wa Ngorongoro,Dk Maurus Msuha alisema magari maalum
yameandaliwa kutoka Arusha hadi Ngorongoro kutembelea vivutio kwa malipo
kidogo.
Post a Comment