Maonesho
ya wakulima na wafugaji nane nane mwaka 2018,yanatumiwa na Taasisi za
uhifadhi kutangaza vivutio vya Utalii nchini na kupiga vita ujangili.
Taasisi
za uhifadhi,Shirika la hifadhi za Taifa(TANAPA),Friedkin conservation
Fund (FCF) na Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro,wameeleza ushiriki wao
katika maonesho ya mwaka huu.
Akizungumza mapema leo,Meneja kitengo cha ujirani Mwema cha shirika la
hifadhi za Taifa(TANAPA),Ahmed Mbugi alisema shirika hilo limejipanga
kutumia maonesho haya kutangaza utalii.
Mbugi
alisema katika maonesho hayo,TANAPA itatoa magari kuwapeleka watalii
hifadhi za taifa za Serengeti kwa washiriki wa maonesho ya kitaifa
mkoani Simiyu.
Alisema kwa wanaoshiriki maonesho mkoa wa Morogoro watapelekwa Hifadhi ya Taifa ya mikumi kwa kuchangia gharama.
Katika
maonesho hayo,pia Taasisi binafsi za uhifadhi zitatoa huduma ikiwepo
taasisi ya Friedkin conservation Fund(FCF) ambayo kwa mara ya kwanza
itashiriki.
Mkurugenzi wa
kampuni ya Mwiba Holdings, moja ya kampuni zilizo chini ya FCF
,Abdukadir Mohamed alisema katika maonesho mwaka huu wameandaa mabanda
ambayo watatoa elimu ya uhifadhi na vita dhidi ya ujangili.
"Pia
tutahamasisha watanzania kwenda kutembelea vivutio vya utalii katika
mapori ya akiba ambayo tumewekeza ikiwepo eneo la makao kwa wakazi wa
kanda ya ziwa" alisema
Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro(NCAA) pia wanatumia maonesho kupeleka watalii wa ndani kuona vivutio vilivyopo Ngorongoro.
Naibu
Mhifadhi Mkuu wa Ngorongoro,Dk Maurus Msuha alisema magari maalum
yameandaliwa kutoka Arusha hadi Ngorongoro kutembelea vivutio kwa malipo
kidogo.
Post a Comment