Mwandishi wetu.
Akizungumza
na watendaji wa Taasisi ya uhifadhi ya Friedkin conservation Fund,(FCF)
inayomiliki kampuni za uwindaji wa kitalii,katika maonesho ya Nanenane
kitaifa mkoa Simiyu,Dk Tzeba alisema kuna kampuni zinapata fedha nyingi
lakini uchangiaji jamii ni ndogo.
"Nyie najua mnafanya vizuri lakini wenzenu katika maeneo mengine hadi wamefikia hatua ya kuwachagulia miradi wananchi" alisema.
Hata
hivyo,Afisa uhusiano wa FCF,Clarence Msafiri alisema kampuni zilizo
chini ya Taasisi hiyo,zimekuwa zikitoa kwa jamii asilimia 20 ya mapato
yao kila mwaka.
Alisema
kampuni zao ikiwepo Mwiba Holding na TGTS na walizowekeza wilayani Meatu
pori la Akiba la Maswa na Makao licha ya kutoa michango ya kijamii pia
kwa mwaka wanatoa kwa vjiji zaidi ya sh 610 million kama kodi ya pango.
Naye
Meneja ujirani Mwema wa kampuni ya Mwiba Holdings Alfred Mwakivike
alisema kampuni hiyo kabla ya kusaidia miradi imekuwa ikipata maelekezo
ya halmashauri.
"Miradi ambayo tunaitekeleza ambayo ina thamani zaidi ya sh 2. bilioni yote imeidhinishwa na halmashauri ya Meatu" alisema.
Taasisi
ya Friedkin inashiriki maonesho ya nanenane kwa mara ya kwanza ili
kuhamasisha uhifadhi,kupiga vita ujangili lakini kuonesha umuhimu wa
mahusiano ya uhifadhi na kilimo.
Post a Comment