Waziri
wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba (Katikati) akisisitiza jambo wakati
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa programu ya
kuendeleza sekta ya kilimo (ASDP II) katika jengo la Mikutano la
kimataifa la Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es salaam, jana 1
June 2018. Wengine ni Katibu Mkuu wizara ya kilimo Mhandisi Mathew
Mtigumwe na Naibu Katibu Mkuu wizara ya kilimo Dkt. Thomas kashililah. Picha zote Na Mathias Canal-WK
Wawakilishi
wa vyombo mbalimbali vya habari wakifatilia mkutano wa Waziri wa Kilimo
Mhe Dkt. Charles Tizeba katika jengo la Mikutano la kimataifa la
Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es salaam, Jana 1 June 2018.
Katibu
Mkuu wizara ya kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe (Kulia), Mratibu wa
ASDP II Mhandisi Januari Kayumbe (katikati) na Kaimu Mkurugenzi wa zana
za kilimo Mhandisi Joseph Lubilo wakifatilia mkutano wa waziri wa kilimo
na waandishi wa habari. Jana 1 June 2018.
Waziri wa Kilimo Mhe Dkt. Charles Tizeba akimsikiliza kwa makini Katibu
Mkuu wa wizara ya kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe wakati wa maandalizi
ya uzinduzi wa programu ya kuendeleza sekta ya kilimo ASDP II katika jengo la Mikutano la kimataifa la Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es salaam, Jana 1 June 2018.
Na Mathias Canal-WK, Dar es salaam
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. John Pombe Magufuli
anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa programu ya
kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili (ASDP II) tarehe 4 June 2018.
Katika
dhifa hiyo inayotarajiwa kuanzia Saa 2.00 asubuhi katika jengo la
Mikutano la kimataifa la Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es
salaam, Rais Magufuli ataambatana na wageni wengine wa kitaifa na
kimataifa akiwemo makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe
Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa, Mkuu wa Mkoa wa
Dara es salaam Mhe Paul Makonda, Mawaziri wa sekta za kilimo pamoja na
wadau wote wa sekta ya hiyo.
Taarifa
ya uzinduzi wa Programu hiyo ya kuendeleza sekta ya kilimo nchini
imetolewa jana 1 June 2018 na waziri wa kilimo Mhe Dkt. Charles Tizeba
wakati akizungumza na waandishi wa habari katika jengo la Mikutano la
kimataifa la Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es salaam.
Dkt
Tizeba alisema, Wizara za kisekta zikijumuisha Wizara ya Kilimo, Wizara
ya Mifugo na Uvuvi, Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za
mitaa-TAMISEMI, Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji, Wizara ya Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Wizara ya Maji na Umwagiliaji ndizo zenye jukumu la kuhakikisha ASDP II inakuwa na mafanikio makubwa nchini na kuwa mkombozi wa wananchi katika kilimo.
Alisema
kuwa ASDP II itatekelezwa katika mikoa na wilaya zote kwa kuzingatia
mazao ya kipaumbele kufuatana na ikolojia ya kilimo ya kanda kwa miaka
kumi (10) kwa vipindi viwili vya miaka mitano mitano ambapo kipindi cha
kwanza kitaanza 2018/19 hadi 2023/24.
Katika
hatua nyingine Dkt Tizeba ametaja lengo la Programu hiyo kuwa ni kuleta
mageuzi katika sekta ya kilimo ili kuongeza uzalishaji na tija katika
kilimo, mifugo na uvuvi; kuongeza pato la wakulima, wafugaji na wavuvi;
kuongeza pato la Taifa na kuwa na uhakika wa usalama wa chakula na
lishe.
Aidha,
Programu hii itatekeleza sera mbalimbali kama vile Sera ya Kilimo ya
Taifa, Sera ya Mifugo ya Taifa, Sera ya Uvuvi, Sera ya Masoko ya Mazao
ya Kilimo, Sera ya Umwagiliaji ya Taifa, Sera ya Usalama wa Chakula na
Lishe, Sera ya Ugatuaji Madaraka, Sera ya Maendeleo ya Ushirika na Sera
ya Mashirikiano kati ya Sekta za Umma na Sekta Binafsi.
Katika
hatua nyingine Mhe Dkt Tizeba ameuarifu umma wa watanzania kuwa endapo
mpango huo utatekelezwa kama ilivyopangwa hadi kufikia mwaka 2022
Tanzania itakuwa katika uchumi wa kati.
Katika
utekelezaji wa ASDP II washiriki ni wadau wa sekta ya Kilimo, Mifugo,
Uvuvi, Ushirika, Wizara, Taasisi za Serikali na zisizo za Serikali,
Washirika wa Maendeleo, Sekta Binafsi na wananchi wote.
Post a Comment