NA: ANDREA NGOBOLE, PMT
Bodi ya wakurugenzi ya mamlaka ya usimamizi wanyamapori nchini (TAWA) imeridhishwa na utendaji wa Makampuni ya uwindaji na upigaji picha za kitalii, ya Mwiba holdings na TGTS yaliyowekeza katika pori la akiba Makao, lilipo mpakani mwa Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro na Meatu.
Wanyama wameongezeka, vita dhidi ya ujangili imefanikiwa na mifugo imedhibitiwa kuingia maeneoya hifadhi lakini pia uchangiaji wa fedha za maendeleo umeongezeka.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa bodi ya TAWA,Meja Jenerali mstaafu Hamisi Semfuko alipotembelea maeneo yaliyowekezwa na kampuni ya mwiba katika eneo la Makao na kitalu Mbono kinachomilikiwa na kampuni ya TGTS.
Amesema kuwa wanyama wameongezeka katika vitalu hivyo vilivyopo wilayani Meatu kutokana na ushirikiano kati ya wawekezaji hao na askari wa Tawa.
Naye Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori nchini (TAWA),
Dk James Wakibara akizungumza na
waandishi wa habari jijini hapa, juu ya mchango kwa jamii, uhifadhi na
kiuchumi wa makampuni ya uwindaji wa kitalii umekuwa na msaada mkubwa kwa maendeleo ya jamii ambapo zimechangia zaidi ya shilingi bilioni 40.
Dk
Wakibara alisema, licha mchango wa makampuni kwenye jamii, pia TAWA
kupitia malipo ya kampuni hizo, imekuwa ikitoa takriban sh 6.5 bilioni
kila mwaka kwa vijiji vyenye wawekezaji hao na halmashauri.
Makampuni
hayo yamewekeza katika baadhi ya maeneo ya vitalu 159 vilivyopo
nchini na maeneo ya hifadhi za jamii za wanyamapori (WMA) 38 zilizopo
nchini.
"Hizi
kampuni za kitalii zina mchango mkubwa sana pia katika uhifadhi wa
maeneo haya, hasa katika vita dhidi ya ujangili ikizingatiwa asilimia 95
ya maeneo yaliyohifadhiwa nchini yapo chini ya TAWA"alisema
Alisema
kwa sasa mapato ya TAWA kutokana na shughuli za uhifadhi, yamefikia
dola 20 lakini kuna mikakati ya kuongeza mapato hayo mara nne zaidi hadi
kufikia dola 80.
"kuna
dhana potofu kuwa uwindaji wa kitalii ni kumaliza wanyama hili sio
kweli, kwani haya makampuni hayajawahi kufikia hata robo kiwango cha
kuwinda wanyama ambacho kinatolewa kila mwaka na TAWA na mashirika ya
kimataifa"alisema
Mwenyekiti
wa bodi ya TAWA,Meja Jenerali mstaafu Hamisi Semfuko alisema mamlaka
hiyo ipo katika mabadiliko makubwa ili kuhakikisha jamii inanufaika
zaidi ya uhifadhi wa wanyamapori,katika kusaidia miradi ya kijamii ya
maji, afya Elimu na uhifadhi.
Mwenyekiti
huyo na bodi yake ambao walitembelea pori la Makao, lilipo mpakani mwa
Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro na Meatu,alisema wameridhishwa na
utendaji wa kampuni ya Mwiba Holding katika eneo hilo.
Kampuni
ya Mwiba holding imewekeza katika hifadhi ya jamii ya wanyamapori(WMA)
ya makao na katika eneo la ranchi katika kijiji cha makao wilayani
Meatu.
Post a Comment