PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: Kijana Aliyemuokoa Mtoto Toka Ghorofani Aanza Kazi Katika Jeshi la Zimamoto
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
      Hadi mwishoni mwa wiki iliyopita maisha ya Mamoudou Gassama, kijana wa Mali mwenye umri wa miaka 22 yalikuwa sawa na ya m...


Kijana Aliyemuokoa Mtoto Toka Ghorofani Aanza Kazi  Katika Jeshi la Zimamoto
Hadi mwishoni mwa wiki iliyopita maisha ya Mamoudou Gassama, kijana wa Mali mwenye umri wa miaka 22 yalikuwa sawa na ya maelfu ya wahamiaji wanaohaha huku na kule barani Ulaya wakitafuta maisha bora.

Ghafla Jumapili nyota ya bahati ilimwangazia Gassama, mambo yalibadilika na kuwa shujaa wa Ufaransa leo. Tukio moja tu la kuokoa maisha ya mtoto limemfungulia bahati na sifa sasa amepewa jina la "Spiderman wa Paris", hadhi kisheria ya kuishi Ufaransa na kufanya kazi katika Jeshi la Zimamoto.

Tukio lililomfanya Gassama, ambaye hadi mwishoni mwa wiki alikuwa mhamiaji haramu lisingefikiriwa kumbadili haraka hivi. Hata hivyo, kuanzia wikiendi hiyo, kijana huyo anaishi maisha ya ndoto yake tangu kumwokoa mtoto wa miaka minne aliyekuwa ananing’inia kwenye kibaraza cha ghorofa ya nne ya jengo.

Kitendo hicho cha kishujaa kimepongezwa nchini kwake Mali na Ufaransa. Jumatatu kijana huyo alipokewa na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na akaahidiwa kupewa uraia ambao Uhamiaji wamekuwa wakishughulikia kuanzia Jumanne. Gassama atapewa kadi ya kibali cha kuishi Ufaransa kwa miaka 10 kabla ya kupewa uraia kamili.

Halafu alikwenda katika Jeshi la Zimamoto la Paris Fire Brigade ambako alitia saini mkataba wa miezi 10. Jumatano alianza mafunzo ya kazi itakayomwezesha kulipwa karibu euro 600 kwa mwezi sawa na shilingi za Tanzania 1,588,990.70

Msanii mashuhuri Rihanna amesema kupitia Instagram: "Nimefurahishwa sana."  Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keïta, mbali ya kumpigia simu kumpongeza ameandika kupitia akaunti ya Twitter: “Mwana mzuri na shujaa wa Mali".

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top