


Akikabidhi vifaa hivyo vyenye thamani ya shilingi milioni 29.8 kwa mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo,mkurugenzi wa kampuni mbili za utalii Kibo Guides na Tanganyika Wilderness Campus ,Willy Chambulo, amesema kampuni zake zitaendelea kuchangia sekta ya afya na elimu .
Kwa upande wake meneja mahusiano wa Hotel ya kitalii ya Mount Meru, Quen Mpeku,ambao wametoa msaada wa Taulo 250 zenye thamani ya shilingi milioni 8
Akipokea msaada huo mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, amesema serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dakt John Magufuli, inaendelea na hatua ya kuboresha huduma ya afya nchini na Jijini Arusha.
Amesema kuwa hivi sasa jiji la Arusha linajenga hospital ya wilaya ambapo Raisi Magufuli amechangia shilingi bilioni 2,huku halmashauri ikiwa imetoa shilingi milioni 500.
Awali mganga mkuu wa mkoa wa Arusha Daktar Timoth Wanyonji, amesema vifaa hivyo vimekabidhiwa kwa timu ya uendeshaji na uboreshaji wa huduma ya afya ya mkoa na jiji la Arusha,ambapo mkakati uliopo ni kuendelea na kupunguza vifo vya wajawazito na watoto wakati wa kujifungua ikiwa ni hatua ya kuboresha huduma ya tiba na kinga.
Amesema vifo vya watoto na akina mama vinaendelea kupungua mwaka hadi mwaka kutokana na kuboresha huduma za afya na kinga.
Ameongeza kuwa jengo la wagonjwa wa nje OPD limekamilika kwa asilimia 90 na bado wanaendelea kukamilisha majengo mengine ikiwemo la chumba cha kuhifadhia maiti, wadi ya kujifungulia, maabara, ambapo yapo ujenzi wake umefikia 50 asilima.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.