Naibu Waziri wa Fedha na Mipango
Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akifunga warsha ya wadau wa Sekta ya Fedha
iliyolenga kujadili mchango wa sekta hiyo katika kukuza uchumi wa
viwanda leo Jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha
na Mipango Dkt. Khatib Kazungu akizungumza wakati wa kufunga warsha ya
wadau wa Sekta ya Fedha iliyolenga kujadili mchango wa sekta hiyo
katika kukuza uchumi wa viwanda leo Jijini Dodoma.
Mbunge wa Jango’mbe Mhe. Ally
Hassan King akizungumza wakati wa kufunga warsha ya wadau wa Sekta ya
Fedha iliyolenga kujadili mchango wa sekta hiyo katika kukuza uchumi wa
viwanda leo Jijini Dodoma.
Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya
Usimamizi wa Bima nchini (TIRA), Dkt. Boghayo Saqware akizungumzia hoja
mbalimbali zilizoibuliwa na wajumbe wa warsha ya wadau wa sekta ya
fedha iliyolenga kujadili mchango wa sekta hiyo katika kukuza uchumi wa
viwanda leo Jijini Dodoma.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe
Dkt. Honest Ngowi akiongoza mjadala wakati wa warsha ya wadau wa sekta
ya fedha iliyolenga kujadili mchango wa sekta hiyo katika kukuza uchumi
wa viwanda leo Jijini Dodoma.
Mmoja wa wadau wa Sekta ya Fedha
akizungumzia umuhimu wa ushirikishwaji wa sekta hiyo katika utekelezaji
wa miradi mikubwa ya maendeleo hapa nchini ili kuchochea maendeleo.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango
…………….
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma
Uamuzi
wa Serikali wa kupunguza kiwango cha chini cha amana kinachotakiwa
kuwekwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na benki za biashara nchini,
umechochea taasisi za fedha yakiwemo mabenki kuanza kupunguza viwango
vya riba ya mikopo hatua itakayochochea ukuaji wa uchumi.
Hayo yalisemwa Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji wakati wa kufunga warsha ya
wadau wa Sekta ya Fedha uliowashirikisha wabunge, washirika wa
Maendeleo, wakuu wa Taasisi za fedha na Wizara ya Fedha na Mipango.
Dkt. Kijaji, alisema kuwa Serikali kupitia Benki
Kuu imeshusha riba ya mikopo kwa taasisi za fedha kutoka asilimia 16.0
hadi asilimia 9.0 na kupunguza kiwango cha chini cha amana
kinachotakiwa kuwekwa katika Benki hiyo na benki za biashara kutoka
asilimia 10.0 hadi asilimia 8.0 kuanzia mwezi Aprili 2017, jambo ambalo limeleta matokeo chanya katika kuimarisha uwezo wa taasisi kukopesha wateja wao.
Miongoni mwa Benki zilizoshusha viwango vyao vya riba za mikopo ni CRDB ambayo
imetangaza kushusha riba kutoka asilimia 22 hadi 16 na kuongeza kiasi
cha kukopa kwa wafanyakazi kutoka Sh. milioni 50 hadi Sh. milioni 100
huku muda wa kurejesha ukiongezwa kutoka miaka mitano hadi saba.
Benki
nyingine ni NMB ambayo imeongeza muda wa marejesho ya mikopo kwa
wafanyakazi, wajasiriamali wadogo na wakubwa kutoka miezi 60 hadi 72,
na imepunguza riba ya mikopo kwa wafanyakazi kutoka asilimia 21 hadi 19
na wajasiriamali wadogo kutoka asilimia 23 hadi 21.
Dkt.
Kijaji amezipongeza benki zilizoshusha viwango vya riba na ameitaja
hatua hiyo kuwa ni muhimu katika kuifikisha Tanzania kuwa nchi ya
viwanda hata kabla ya mwaka 2025 na kutoa wito kwa taasisi hizo za fedha
kuitupia jicho sekta ya kilimo kutokana na umuhimu wake katika kutimiza
malengo ya kukuza viwanda.
Aidha, Dkt. Kijaji alisema kuwa Serikali imekamilisha andiko “Blue Print”
ambalo lengo lake ni kuboresha mazingira ya kufanya biashara nchini
ili kuleta tija kwa wafanyabiashara na Sekta ya Fedha kwa ujumla
Alisema
Serikali imeendelea kulipa malimbikizo ya madai mbalimbali
yaliyohakikiwa ya watumishi, wakandarasi na watoa huduma wengine
yaliyohakikiwa ili kuongeza ukwasi katika jamii na kwa kwamba uhakiki
uliofanyika umeokoa kiasi kikubwa cha fedha za Serikali ambazo
zingelipwa wakati madai hayakuwa sahihi.
Naibu
Waziri huyo aliipongeza Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa kushiriki kwa
vitengo katika utekelezaji wa Mpango huo kwa kutekeleza miradi ya
kimkakati ya kilimo cha miwa na uzalishaji wa sukari katika eneo la
Mkulazi na Mbigiri – Morogoro na mradi wa ujenzi wa machinjio ya kisasa
ya nyama eneo la Makunganya mkoani humo.
Naye
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu,
alieleza kuwa warsha hiyo iikuwa na manufaa makubwa na kwamba Wizara
inaandaa mkakati wa utekelezaji wa Sekta ya Fedha wa Miaka kumi ambao
utakujumuisha pia mawazo ya wadau hao.
Kwa
upande wake Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Prof. Honest Ngowi,
amepongeza hatua ya Serikali ya kuwa na majadiliano na Sekta ya fedha
kwa kuwa ina mchango mkubwa katika kutekeleza Mpango wa Pili wa
Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano.
Akitoa
tathimini yake kuhusu utekelezaji wa Mpango huo, Prof. Ngowi, alisema
kuwa sehemu ya miradi kumi ya kipaumbele, ikiwemo ujenzi wa Reli ya Kati
kwa kiwango cha Kimataifa (SGR), ufufuaji wa Shirika la Ndege na Ujenzi
wa Kiwanda cha Sukari Mkulazi mkoani Morogoro, ni baadhi ya miradi
muhimu inayotekelezwa.
Kwa Upande wao, Mbunge wa Muheza Mhe. Adadi Rajab na Mbunge
wa Viti Maalum Mhe. Maria Kangoye, wamezishauri Sekta za Fedha nchini
kuiwezesha zaidi sekta ya kilimo ili ikue haraka na kuishauri pia Wizara
ya Fedha na Mipango, kufanya mikutano ya namna hiyo na wadau kabla ya
Bunge la Bajeti kuanza ii manufaa yake yaweze kuwa makubwa zaidi.
Post a Comment