Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma
Rais
wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, Dkt. Akinumwi Adesina, amesema
Benki hiyo imeridhishwa na utekelzaji wa miradi ya nishati hapa nchini
kwani inachochea mageuzi katika maisha ya wananchi .
Akizungumza
mara baada ya kuwasili Mkoani Dodoma na kutembelea kituo cha kupoza
umeme cha Zuzu, mkoani Dodoma, amesema kuwa benki hiyo inatambua na
kupongeza juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt.
John Pombe Magufuli katika kusukuma mbele kurudumu la maendeleo.
Dkt.
Adesina ameeleza kuwa ujenzi wa kituo hicho cha kupoza umeme ni mkakati
wa Serikali ya Awamu ya Tano ya kuondoa changamoto ya upatikanaji wa
nishati ya umeme kwa wananchi wake na umelenga pia kupunguza tatizo la
upatikanaji wa umeme katika nchi jirani zinazopakana na Tanzania ikiwemo
Burundi na Kenya.
Alisema
kuwa katika kuhakikisha mpango huo wa kupeleka umeme huo na kuunganisha
na nchi jirani, Benki yake imetoa kiasi cha dola za Marekani milioni 75
kufanikisha mradi huo wenye thamani ya zaidi ya dola milioni 220.
"Umeme
ni jambo muhimu sana katika maendeleo ni sawa na damu katika mwili wa
binadamu, ukiwa na damu mwilini unakuwa na hai kama huna unakufa! kwa
hiyo uchumi bila umeme wa uhakika hauwezi kushamiri" alisisitiza Dkt.
Adesina
Aliahidi
kuwa Benki yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kukuza
maendeleo ambapo hivi sasa Benki yake iko katika mazungumzo na Serikali
ili mkopo nafuu wa dola za Marekani milioni 165 uweze kupatikana kwa
ajili ya kujenga mradi wa nishati ya umeme katika ukanda wa Kaskazini
Magharibi mwa nchi.
"Vile
vile tutawasilisha kwenye Bodi ya Wakurugenzi wa Benki yetu ili kiasi
cha dola za Marekani milioni 45 kinachoombwa na Serikali kwa ajili ya
kujenga mradi wa umeme unaotokana na joto ardhi uweze kupatikana ili
kuboresha na kuwa na umeme wa uhakika nchini kwa ajili ya kusukuma
maendeleo ya viwanda nchini" alisema Dkt. Adesina
Alisema
kuwa kwa ujumla Benki yake katika kipindi cha miaka miwili ijayo
(2018/2019 na 2019/2020) Benki yake itatoa kiasi cha dola za Marekani
bilioni 1.5 katika sekta ya umeme na kueleza matumaini yake kwamba hatua
hiyo itawawezesha wazalishaji mali wadogo, wa kati na wakubwa kuzalisha
bidhaa na mali mbalimbali na hivyo kukuza uchumi wao na wa Taifa kwa
ujumla.
Kituo
cha kupoza umeme zuzu ni sehemu ya mradi wa umeme unaonufaisha mikoa ya
Iringa, Dodoma, Singida na Shinyanga ambapo vijiji zaidi ya 121
vimeshanufaika na maradi huo wa uzalishaji na usambazaji wa umeme kwa
mikoa husika.
Alisema
kuwa miradi inayoendelea hivi sasa nchini Tanzania kupitia ufadhili wa
Benki yake imefikia thamani ya zaidi ya dola za Marekani bilioni 2
ambapo uwekezaji mkubwa uko katika sekta za nishati ya umeme, usafiri,
miundombinu ya barabara, kilimo, maji na usafi wa mazingira, kusaidia
Bajeti Kuu ya Serikali pamoja na uendelezaji wa rasilimali watu.
Kwa
upande wake, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amesema
kuwa Serikali ya Tanzania inashukuru kuwa Benki ya Maendeleo ya Afrika
ni mshirika mkubwa wa Maendeleo wa Tanzania kutokana na kusaidia
Serikali katika uwekezaji mkubwa unaogusa nyanja mbalimbali ikiwemo
nishati na miundo mbinu mingine kama barabara.
Aliongeza
kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na Benki hiyo katika kuwaletea
wananchi maendeleo ya kweli kwa kuwa hiyo ndio dhamira ya Serikali ya
Awamu ya Tano.
Kwa
upande wake Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu amesema kuwa
Benki hiyo ni mshirika wa kweli katika sekta ya nishati na imewezesha
kufanikiwa kwa miradi mbalimbali ya umeme ukiwemo ule unaoinifaisha
mikoa ya Iringa, Singida, Dodoma, Shinyanga na Dodoma.
Miradi
inayotekelezwa hapa nchini kwa sasa kupitia ufadhili wa Benki ya AfDB
imefikia zaidi ya dola za Marekani bilioni 2 ambapo uwekezaji mkubwa
uko katika sekta za nishati ya umeme, usafiri, miundombinu ya barabara,
kilimo, maji na usafi wa mazingira, kusaidia Bajeti Kuu ya Serikali
pamoja na uendelezaji wa rasilimali watu.
Ushirikiano
wa AfDB na Tanzania ulianza tangu mwaka 1971 na mpaka sasa benki hiyo
imeipatia Tanzania kiasi cha dola za Marekani bilioni 3.6, karibu
shilingi trilioni 8 za Tanzania.
Rais wa AfDB yuko nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kwa mwaliko wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira
Mgalu akisalimiana na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina mara baada ya kuwasili mjini
Dodoma ambapo alitembelea na kukagua mradi wa kituo cha kupoza umeme cha zuzu mkoani humo .
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip
Isdori Mpango ( Mb) akimuongoza
Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina mara baada ya kuwasili mjini
Dodoma ambapo alitembelea na kukagua
mradi wa kituo cha kupoza umeme cha zuzu
mkoani humo.
Rais wa wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina akisalimiana na
Mhandisi Peter Kigadi mara baada ya kuwasili mjini Dodoma
ambapo alitembelea na kukagua mradi wa kituo cha kupoza umeme cha Zuzu mkoani humo .
Rais wa wa Benki ya Maendeleo ya Afrika
(AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina
akisisisitiza jinsi Benki hiyo inavyoridhishwa na hatua mbalimbali
zinazochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John
Pombe Magufuli katika kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa
nishati hali itakayochochea maendeleo.
Mhandisi Mkuu wa Kituo cha kupoza umeme cha Zuzu, Mkoani Dodoma Bw. Joseph
Mongi akitoa maelezo kuhusu namna kituo hicho kinavyofanya kazi wakati wa ziara
ya Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika
(AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina katika kituo
hicho.
Sehemu ya Miundombinu ya kituo cha kupoza umeme cha Zuzu kilichoko mkoani
Dodoma kama inavyoonekana.
Rais wa wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina akiwa kwenye picha ya pamoja
na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdori Mpango (Mb) na Naibu
Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip
Isdori Mpango (Mb) na Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu, wakimuongoza Rais wa wa Benki ya Maendeleo ya Afrika
(AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina kukagua
miundombinu ya Kituo cha kupoza umeme cha Zuzu, mjini Dodoma.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano-Wizara ya Fedha na Mipango)
Post a Comment