PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: Waziri Tizeba, Mpina Matatani kwa Kutohudhuria Mkutano wa Rais IKULU
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
    Waziri wa Kilimo, Dk Charles Tizeba na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina pamoja na Makatibu wao wameshindwa kuhudhuri...


Waziri wa Kilimo, Dk Charles Tizeba na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina pamoja na Makatibu wao wameshindwa kuhudhuria mkutano wa 11 wa baraza la taifa la Biashara uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam na kuendeshwa na Rais Dkt Magufuli.

Katika mkutano huo Rais Magufuli aliwahitaji mawaziri hao ili waweze kutoa ufafanuzi kuhusu maswala ambayo yameibuliwa na wafanyabiashara, lakini mawaziri hao pamoja na Makatibu wao hawakufika licha ya kuwa walialikwa na kupaswa kuwepo kwenye mkutano huo.

Kufuatia kutokuwepo kwa viongozi hao, Rais Magufuli alimuuliza Waziri Mkuu (Kassim Majaliwa) kama waliweza kuwaalika mawaziri hao na ndipo Waziri Mkuu alipojibu kuwa walipata mualiko na walipaswa kuwepo kwenye mkutano huo ingawa hakukuwa na taarifa yoyote ya wao kutokuwepo wala kutuma wawakilishi wao.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top