PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: DIWANI MAARUFU KATA YA KALOLENI ARUSHA AJIUZULU CHADEMA AJIUNGA CCM
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
      Diwani wa chadema ,Kata ya Kaloleni ,jijini Arusha ,Emanuel Kessy amejivua wadhifa wake na kujiunga na ...

 

Diwani wa chadema ,Kata ya Kaloleni ,jijini Arusha ,Emanuel Kessy amejivua wadhifa wake na kujiunga na ccm Kwa kile alichodai ni kumuunga mkono rais John Magufuli

Kessy Ambaye Amekuwa akitajwa na chadema kuwa ni miongoni  mwa madiwani wenye mpango wa kukihama chama chao ,Jana machi 19 ,Ametangaza kuachia ngazi usiku wa Manane baada ya mke wake kumtilia ngumu .

Kessy pia amejivua uanachana wa chadema  na kutimkia ccm huku taarifa zikieleza kwamba mke wake alikuwa ni kikwazo kuachia ngazi Kwa mumewe hata hivyo baadaye ilifanikiwa kumrubuni na hatimaye ilipofika majira ya usiku alilegea na kukubali mumewe aachie ngazi

Wakati kukiwa na taarifa hiyo iliyofanya idadi ya madiwani wa chadema jijini hapa kutimkia ccm kufikia 6,uongozi wa chadema mkoani hapa umekitupia lawama kikundi cha wanaccm wanaoendesha mpango wa kuwarubuni madiwani wao .

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top