Picha Zote Na Mathias Canal
Naibu
Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Dotto Mashaka Biteko akikagua mtambo wa
uchongaji mashimo kwa ajili ya utafiti wakati alipotembelea Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Mtaa wa Upanga Jijini Dar es salaam, Leo 16 Januari 2018.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Dotto Mashaka Biteko akisisitiza uwajibikaji wakati wa
kikao cha pamoja na Uongozi pamoja na watumishi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Mtaa wa Upanga Jijini Dar es salaam, Leo 16 Januari 2018.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Dotto Mashaka Biteko akisisitiza jambo wakati wa
kikao cha pamoja na Uongozi pamoja na watumishi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Mtaa wa Upanga Jijini Dar es salaam, Leo 16 Januari 2018.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Dotto Mashaka Biteko akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Mtaa wa Upanga Jijini Dar es salaam, Leo 16 Januari 2018.
Na Mathias Canal, Dar es salaam
Uongozi
wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) umetakiwa kutoa maelezo kwa
serikali katika kipindi cha muda mfupi kueleza sababu za kuendelea
kusalia kuwepo kwa shirika hilo kutokana na kukosa umakini katika
utendaji.
Kauli
ya kuchukizwa na utendaji wa Shirika hilo imetolewa Leo 16 Januari 2018
na Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Dotto Mashaka Biteko Wakati
akizungumza na Uongozi pamoja na watumishi wa Shirika hilo Mtaa wa
Upanga Jijini Dar es salaam.
Mhe
Biteko alisema kuwa serikali ilikuwa na makusudi mazuri kufuatia
mabadiliko ya Sera za kiuchumi katika miaka ya 1980 kwa STAMICO kuwekwa
kwenye orodha ya mashirika yanayotakiwa kubinafsishwa na hatimaye
kubinafsishwa rasmi mwaka 1996 lakini katika kipindi chote cha utendaji
hakuna msaada wowote ambao Shirika hilo limeipatia serikali zaidi ya
kuingiza hasara maradufu.
Alisema
kuwa pamoja na STAMICO kuwa na jukumu la kuendeleza migodi ya Madini na
kufanya biashara za Madini ikiwemo mradi wa dhahabu wa STAMIGOLD uliopo
Biharamlo Mkoani Kagera na Mgodi wa Makaa ya Mawe KABULO uliopo Mkoani
Ruvuma lakini Taasisi hiyo imeshindwa kuendeleza migodi kwa ufanisi huku
wachimbaji wadogo wakisalia kuwa katika uduni wa mbinu rafiki na tija
katika utendaji kazi wao.
Alisema
kuwa Shirika hilo linapaswa kutafakari kwa umakini utendaji wake kwani
limeongeza hasara kwa serikali ya deni la shilingi Bilioni 1.77 hivyo
serikali haiwezi kuendelea kusalia kuwa na Shirika linalozalisha madeni
kuliko matokeo makubwa na faida.
Aliongeza
kuwa wataalamu wote katika sekta ya Madini wanapaswa kutambua kuwa
biashara ya Madini ni zaidi ya kutoa leseni hivyo watambue kuwa kuna
kila sababu ya kuwa na matumizi bora ya mapato na kutazama namna bora ya
kuifanya sekta ya Madini kuchangia asilimia 10% ya pato la Taifa.
Mhe
Biteko alisema kuwa imani bila matendo ni uduni wa fikra hivyo kuwa na
cheo kikubwa serikalini halafu uzalishaji ni mdogo ni kipimo halisi cha
utendaji wa mazoea walionao watumishi wengi ambao wamekosa uzalendo na
bidii katika utendaji kazi.
Alisema
kuwa serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli imekusudia kusimamia
vyema rasilimali za wananchi hivyo watendaji katika sekta mbalimbali
wanatakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kumsaidia Rais Magufuli katika
kuteleleza adhma ya serikali.
Post a Comment