PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: KIKAO KAZI CHA 13 CHA MAAFISA HABARI, MAWASILIANO, UHUSIANO NA ITIFAKI SERIKALINI KUFANYIKA JIJINI ARUSHA MARCH 12
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Mwenyekiti wa chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) katikati Bwana Paschal Shelutete uhusiano akizungumza na wanaha...
Mwenyekiti wa chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) katikati Bwana Paschal Shelutete uhusiano akizungumza na wanahabari juu ya kikao kazi cha 13 cha maafisa habari, mawasiliano, uhusiano na itifaki serikalini kinachotarajiwa kufanyika 12-16 march 2018 jijini Arusha.
 Mwenyekiti wa chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) Paschal Shelutete uhusiano akizungumza na wanahabari juu ya kikao kazi cha 13 cha maafisa habari, mawasiliano, uhusiano na itifaki serikalini kinachotarajiwa kufanyika 12-16 march 2018 jijini Arusha.



NA: ANDREA NGOBOLE PMT

ZAIDI ya maafisa habari na mawasiliano serikalini 300 wanatarajia kukutana jijini Arusha katika kikao kazi chenye lengo la kuwajengea uwezo wa namna ya kutangaza shughuli za serikali ili kuendana na kasi ya utendaji wa serikali ya awamu ya tano.

Kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa na mwenyekiti wa chama cha maafisa habari na mawasiliano serikalini Pascal Shelutete imesema kuwa kikao kazi hicho kinatarajiwa kufanyika mnamo tarehe 12 -16, march 2018 jijini Arusha, ambapo jumla ya maofisa habari na mawasiliano 300 wanatarajiwa kushiriki katika kikao kazi hicho.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa jumla ya mada 14 zinatarajiwa kuwasilishwa na wataalamu watakaoleta uzoefu mpana katika mawasiliano na kujenga mjadala chanya na fursa ya kubadilisha uzoefu kati ya maafisa mawasiliano na wadau wengine wa tasnia ya habari nchini.

Kikao kazi hicho kimeandaliwa na chama cha maafisa habari na mawasiliano serikalini (TAGCO) kwa kushirikiana na wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambapo kitashirikisha wanachama wote toka kila wizara, idara zinazojitegemea, taasisi na wakala wa serikali(MDAs) ambapo maafisa habari na  mawasiliano wamehimizwa kuthibitisha ushiriki wao kabla ya march 7 mwaka huu 2018.




TAGCO ni chama kilichoanzishwa rasmi mwaka 21012 na kusajiliwa kwa mujibu wa sheria za nchi ambapo kila mtumishi wa umma anayeshughulika na masuala ya habari na mawasiliano anapaswa kuwa mwanachama wa TAGCO.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top