Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Godbless Lema amempongeza Rais John Magufuli kwa kutoa msamaha kwa wafungwa.
Pia, amemshauri kuwaangalia mahabusu waliokaa muda mrefu gerezani pasipo kupata haki.
Katika maadhimisho ya uhuru wa Tanganyika (Tanzania Bara) jana Jumamosi
Desemba 9,2017mkoani Dodoma, Rais Magufuli alitoa msamaha kwa wafungwa
8,157 kati yao 1,828 waliachiwa huru kuanzia jana.
Rais John Magufuli, Jumapili Desemba 10,2017 ametia saini nyaraka za
msamaha alioutoa kwa wafungwa 61 waliohukumiwa kunyongwa hadi kufa na
wawili Nguza Viking na Johnson Nguza (Papii Kocha) waliohukumiwa kifungo
cha maisha jela.
Akizungumza na MCL Digital, Lema amesema kuna mateso wanayopata mahabusu ambayo yanahitaji kuangaliwa.
“Rais Magufuli, Mungu akubariki kwa msamaha uliotoa jana kwa wafungwa na
hasa wale waliokaa magereza muda mrefu pamoja na wazee, msamaha ni
ibada,” amesema Lema ambaye pia ni mbunge wa Arusha Mjini (Chadema).
“Ni msamaha muhimu kwao, mtu aliyehukumiwa maisha au kifo akipata
msamaha ni jambo jema sana, ninafurahi wamesamehewa sasa hawatakuwa tena
magereza maisha yao yote,” amesema.
Lema amesema, “Nimefurahi kwamba hata wale waliokuwa wamehukumiwa
kunyongwa hasa wazee pia wamepata msamaha, kwangu ninaona ni jambo jema
na zuri, kwa mtu anayejua huzuni ya magereza atakubaliana nami.”
Kuhusu mahabusu, Lema amesema, ‘’Wako mahabusu wamekuwa magereza kwa
muda mrefu bila kesi zao kukamilika. Mheshimiwa Rais fuatilia watu kama
hawa pia.”
By Ibrahim Yamola, Mwananchi
About Author
Journalist , Enterpreneur, Lecturer and Blogger. Email :ngoboleaa@gmail.com.
Advertisement
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment