Wagombea 42 wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wamechuana katika kura ya maoni
kuomba kuteuliwa kuwania ubunge wa Singida Kaskazini na Songea Mjini
katika mikutano iliyofanyika leo.
Uchaguzi katika majimbo hayo unafanyika baada ya mbunge wa Songea Mjini,
Leonidas Gama wa CCM kufariki dunia Novemba 24,2017; huku Singida
Kaskazini aliyekuwa mbunge, Lazaro Nyalandu akijivua uanachama wa CCM na
kujiunga na Chadema.
Katika mkutano wa uchaguzi Songea Mjini uliofanyika leo Desemba 10,2017
Msimamizi wa uchaguzi, Palolet Mgema amesema wagombea walikuwa 20 na
wapiga kura walikuwa 605. Amemtangaza John Nchimbi kuwa mshindi kwa
kupata kura 219.
John amewashinda wapinzani wake wa karibu ambao ni waziri wa zamani Dk
Terezya Huvisa aliyepata kura 181 na mwanasheria Dk Damas Ndumbaro
aliyepata kura 83.
Jimbo la Singida Kaskazini, msimamizi wa uchaguzi Athuman Hamad
amemtangaza Haider Hussein Gulamali kuwa mshindi baada ya kupata kura
606 kati ya kura 1,010 zilizopigwa sawa na ushindi wa asilimia 60.
Miongoni mwa wengine 21 waliomfuatia Gulamali ni Justine Monko aliyepata
kura 133 na Juma Mgoo aliyekuwa mkurugenzi mkuu huduma za misitu
amepata kura 46.
Nchimbi, Gulamali Waibuka Kidedea Kura ya Maoni
Title: Nchimbi, Gulamali Waibuka Kidedea Kura ya Maoni
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Wagombea 42 wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wamechuana katika kura ya maoni kuomba kuteuliwa kuwania ubunge wa Singida Kaskazini na Songea M...
Post a Comment