PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: HABARI PICHA WANAHABARI WALIVYOUNGANA NA MKUU WA MAJESHI MSTAAFU GEORGE WAITARA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO SIKU YA UHURU DESEMBA 9, 2017
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Maandalizi ya wanahabari wakiongozwa na Meneja Mawasialino wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Paschal Shelutete akihojiwa t...


Maandalizi ya wanahabari wakiongozwa na Meneja Mawasialino wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Paschal Shelutete akihojiwa tayari kwa kuanza safari hapa ni Hotel ya Zara iliyopo mkoani Kilimanjaro 
 Kundi la Wahabari 15 wakiwa katika picha ya pamoja geti la Marangu ikiwa ni muda mfupi kabla safari kuanza kuelekea Kilele cha Uhuru cha mlima mrefu kuliko yote barani Afrika wa Kilimanjaro.
Madaktari wa Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro (KINAPA) hawakuwa nyuma kuhakikisha kila mwenye tashwishwi anatibiwa haraka hapa ni mwanahabari Dikson Busagaga wa clouds media group akipatiwa matibabu ya goti
 Mapumziko  pia yaliruhusiwa hapa wanaonekana waandishi Bertha Mwambela mwenye truck suit ya kijivu na  mistari meupe wa TBC Tanga, jamila Omari wa chanel ten Arusha mwenye koti jekundu na kulia kabisa ni Pascal shelutete meneja mawasiliano wa TANAPA.
Kufurahia pia kulikuwamo ili kuondoa uchovu na maumivu ya kupanda Mlima Kilimanjaro kama wanavyoonekana wanahabari BERTHA MWAMBELA, MUSSA JUMA NA JAMILA OMARI wakifurahi.
 Mwandisho wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten Arusha Jamila Omar alionekana kuitawala safari na hata kulazimika kuimba wakati wote kama anavyoonekana
Muhifadhi Mkuu wa KINAPA  Betty Loiboki naye hakuwa nyuma katika safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro
Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Mwananchi Arusha Mussa Juma na Mwandishi wa Gazeti la MTANZANIA Arusha Eliya Mbonea  


Wanahabari Jamila Omar katikati, Mussa Juma kushoto na Eliya Mbonea wakiwa wamewasili kituo cha Horombo
 Mwandishi Eliya Mbonea kushoto akiwa katika ;picha ya pamoja na Luteni Lugano Mwakagugu 
 Mwanahabari kutoka Tanga Betha Mwambelwa kushoto, akifuatiwa na Meneja Mawasiliano wa TANAPA Paschal Shelutete wakisikiliza maelekezo kutoka kwa  kiongozi wa msafara  
Luteni Mwakagugu mwenye Bendera ya Taifa akitoa maelekezo kwa wanahabari Jamila Omar na Mussa Juma kwenye eneo la utalii lijulikanalo kama Zebra Rocky yaani miamba iliyojichora kama mnyama pundamilia hakika ilipendeza sana na wanahabari walifurahia sana trip hiyo ya kihistoria.
Wanahabari kutoka kushoto ni Jamila Omary, muhifadhi wa KINAPA Elisante Mussa Juma, Eliya Mbonea, Anne Robbi na Dotto Aristide wakiwa katika eneo la Zebra Rocky
 Safari ya kuelekea kileleni ikiendelea 

 Mwanahabari Dotto akiendelea kupasua anga 
Meneja Mawasiliano wa TANAPA Shelutete mwenye kofia akiafuatiwa na mwanahabari George Mbara wa ITV Dodoma nyuma 

Askari wa JWTZ Dyness mwenye Tshirt ya njano akifurahia jambo na baadhi ya waandishi wa habari

wasaidizi wa wapanda mlima wajulikano kama porters wakiwajibika ipasavyo kuhakikisha kuwa mambo yanakwenda sawa

katikakati ya safari lazima mpumzike kwa ajili ya lunch ili kurejesha nguvu iliyopotea ukiwa safarini hapa ni Jamila Omari na Elia Mbonea wakipata chakula cha mchana katika moja ya mapumziko wakielekea kituo cha Kibo

kuelekea kilele cha uhuru wanahabari Mussa Juma wa gazeti la mwananchi Arusha  mwenye koti jeupe na Jackline massano wa gazeti la Uhuru Daresalaam wakielekea kilele cha Uhuru juu kabisa ya mlima Kilimanjaro

 Mwanahabari Eliya Mbonea akiongoza msafara kuelekea Kilele cha Uhuru 
 Mwanahabari Jackline Massano akiwa katika Kilele cha Stella na aliyekaa menye koti jekundu ni askari wa JWTZ
 Mwanahabari Mussa Juma na Eliya Mbonea wakiwa katika Kilele cha UHURU cha Mlima Kilimanjaro 

Wanahabari Andrew Ngobole kushoto wa princemedia TZ na chuo cha habari fanikiwa, Robert Mayungu wa Azam TV Morogoro  na Dixson Busagaga wa clouds media group kilimanjaro kulia mara baada ya kutelemka Mlima Kilimanjaro 
 Baadhi ya wanahabari wakiendelea kubadilishana mawazo mara baada ya kushuka kutoka mlima kilimanjaro wakijiandaa kupokelewa katika geti kuu la marangu kulia kabisa ni mkuu wa hifadhi ya Kilimanjaro LOIBOOKI
 Meneja Mawasilianiwa TANAPA Paschal Shelutete akiteta jambo na Chief Guide Faustine Chombo kutoka Kampuni ya Utalii ya Zara mara baada ya kushuka kutoka Mlima Kilimanjaro  

 Mwanahabari Jamila Omar akiteta jambo na Mkuu wa Majeshi Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi ya TANAPA Jenerali George Waitara mara baada ya kutelemka Mlima Kilimanjaro 
Mwandishi Charles Ndagula akiendelea na marekebisho mara baada ya kufanikiwa kutelemka Mlima Kilimanjaro
 Furaha ilitawala kutoka kwa wapanda mlima wakipokelewa katika lango kuu la Marangu

 Ilikuwa ni furaha na shangwe kushuka Mlima Kilimanjaro 

 Hotuba ikifuatiliwa kwa umakini na wanahabari
Wanahabari wakifuatilia kwa makini hotuba zilizotolewa wakati wa mapokezi ya wapanda Mlima Kilimanjaro 
 Wanahabari kutoka Mkoani Kilimanjaro nao walifika kujumuika kuwapokea wanahabari, askari wa Jeshi la Wananchi, Maofisa wa KINAPA, Maofisa kutoka Chama cha Urafiki wa Tanzania na China waliokuwa wamepanda Mlima Kilimanjaro 
 Wanahabari Mark Nkwame kulia, Anne Robbi katikati na Betha Mwambela wakijadiliana jambo 
 Chief Guide kutoka Kampuni ya Zara Faustine Chombo akihojiwa na wanahabari 
Chief Guide kutoka Kampuni ya Zara Faustine Chombo akimkabidhi mwanahabari Jamila Omar Vyeti vya wanahabari waliopanda Mlima Kilimanjaro

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top