Chama cha ACT- Wazalendo kitakutana Ijumaa Oktoba 20, 2017 kujadili
masuala kadhaa, likiwemo la kujizulu kwa mwenyekiti wake wa Kamati ya
Kampeni na Uchaguzi Taifa na Mjumbe wa Kamati Kuu, Samson Mwigamba.
Mwigamba jana Jumatatu, Oktoba 16 ameandika barua ya kujizulu uongozi na
kueleza atabaki kuwa mwanachama wa kawaida ili aweze kupata fursa ya
kuwahoji kwa matendo viongozi.
"Nimeamua kukaa kando kwa kuwa tumekuwa hatukubaliani na baadhi ya mambo
ndani ya chama na hasa kiongozi wetu… wacha nikae pembeni niwe
mwanachama ili niwe na nafasi ya kuwahoji vizuri viongozi wetu masuala
mbalimbali na nitabaki kuwa mwanachama mwema,’’ amesema alipozungumza na
Mwananchi.
Akizungumzia uamuzi huo, Kiongozi wa chama hicho, Zitto Kabwe amesema,
“Nimepokea barua yake. Tutatafakari suala hilo na masuala mengine
yanayohusiana na hayo kwenye kikao cha Kamati ya Uongozi wa chama
Ijumaa.”
“Ndugu Mwigamba ataalikwa kwenye kikao hicho. Ninamshukuru sana kwa
utumishi wake uliotukuka kwenye chama na ninamtakia kila la kheri.
Mchango wake na kujitoa kwake kwa hali na mali hakutasahaulika kwenye
chama chetu,” amesema Zitto.
Home
»
KITAIFA
»
Matukio
»
Siasa
» Zitto Kabwe athibitisha kupokea barua ya kujiuzuru Samson Mwigamba
About Author
Journalist , Enterpreneur, Lecturer and Blogger. Email :ngoboleaa@gmail.com.
Advertisement
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment