Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akitoa nasaha kwa wachezaji wa mpira wa pete TASWA QUEENS DSM na TASWA ARUSHA QUEENS katika mchezo ulioisha kwa Taswa queens DSM kujinyakulia ushindi mnono |
Mwenyekiti wa Taswa FC Majuto Omari akizungumza na wanahabari waliojitokeza katika tamasha la wanahabari mkoani Arusha lililofanyika katika viwanja vya general tyre. |
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho gambo akikagua timu ya Sunrise radio kabla ya mchezo wao na radio Five katika tamasha la wanahabari mkoani Arusha |
Timu
ya mpira wa miguu ya waandishi wa habari za michezo nchini (Taswa FC)
na ya mpira wa pete (Taswa Queens) zimetwaa ubingwa wa tamasha la 13 la
vyombo vya habari la Arusha (Arusha Media Bonaza) lililofanyika kwenye
viwanja vya General Tyre.
Wakati
Taswa FC ikitwaa nafasi ya kwanza kwa mpira wa miguu baada ya
kujikusanyia pointi saba, Taswa Queens ilitwaa nafasi ya kwanza kwa
upande wa netiboli baada ya kuifunga Taswa Arusha kwa mabao 19-7 katika
mchezo wa kusisimua ulioshuhudiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho
Gambo.
Akizungumza katika ufunguzi wa tamasha hilo mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema kuwa michezo ni afya na ajira kwa vijana wengi kwa sasa na wanahabari kama tasnia inayounganisha jamii kubwa haina budi kuendeleza michezo mbalimbali ili kuhakikisha jamii inapata uelewa wa kutosha juu kukuza na kuendeleza vipaji vyao.
Aliipongeza taswa fc na taswa queens kwa kuleta changamoto katika tamasha hilo na kiziasa timu za vyombo vya habari Arusha kujenga utamaduni wa kuwa na michezo ya mara kwa mara ili kujiweka fiti muda wote vinginevyo watakuwa wakifungwa kila tamasha la wanahabari linapofanyika na kuwaachia taswa fc na taswa queens kutoka Daresalaam kujinyakulia ushindi huo mara kwa mara.
Aidha ametoa changamoto kwa kamati ya maaandalizi ya bonanza hilo kuangalia namna ya kuliboresha bonanza hili kwa kuongeza timu nyingine kama za serikali ya mkoa, watu wa bodaboda na tasnia nyingine ili kuleta mshikamano jijini Arusha.
Mwenyekiti
wa Taswa Arusha Jamila Omari amemshukuru mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho
Gambo kwa kuukubali mwaliko wa kuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo na
nasaha alizotoa kwa wanahabari mkoani Arusha kuwa wazingatie kufanya
mazoezi ya mara kwa mara uli wawe na afya bora na wasisubiri mpaka bonanza
ndiyo wacheze mpira.
Katibu
Mkuu wa Taswa Arusha, Mussa Juma alizipongeza timu zote kwa kushiriki
katika bonanza hilo ambalo lilidhaminiwa na Hifadhi za Taifa (TANAPA)
Mifuko ya hifadhi ya Jamii ya LAPF na PSPF, Mamlaka ya hifadhi ya
Ngorongoro, kampuni ya bonite botllers LTD kupitia kinywaji chake cha Coca Cola, Tanzania breweries LTD, kampuni ya ya vinywaji baridi ya SBC (T) Limited kupitia kinywaji chake cha Evervess
na Arusha Palace Hotel ambapo alitaja timu zilizoshiriki katika tamsha hilo kuwa ni waandaji wenyeji wa tamasha hilo Taswa Arusha, Sunrise radio, Radio five Arusha na wageni pekee timu ya Taswa fc kutoka Daresalaam
Mbali
ya Taswa FC kutoka Daresalaam kutwaa vikombe vya mpira wa miguu, timu hizo ambazo zinadhaminiwa na
kampuni ya MultiChoice Tanzania (DSTV), benki ya TPB na Property
International Limited, pia ilihakikisha vyombo vya ha ari vya Arusha
vinaondoka mikono mitupu baada ya kutwaa nafasi ya kwanza katika mbio
za kufukuza kuku. Magret Elia ambaye ashinda kuku wawili na Veronica
Deus aliyeshinda mara moja.
Taswa
FC ilianza kampeni yake kutetea ubingwa wake kwa kutoka sare ya 1-1
dhidi ya Radio Sun Rise. Timu hiyo ilisawazisha kupitia kwa Zahoro
Mlanzi baada ya gonga safi za Wilbert Molandi, Ali Salum na Saidi
Seif.
Taswa
FC ilibadili upepo wa mashindano hayo baada ya ushindi wa mabao 2-0
dhidi ya Taswa Arusha baada ya Ibrahim “Maestro” Masoud kufunga kwa
penati na Nicholas Ndifwa kufunga la pili baada ya ushirikiano mzuri wa
Martin Shilla, Edward Mbaga, Kulwa Ndege na Muhidin Sufiani.
Mchezo
wa kuamua nani bingwa ulikuwa kati ya Taswa SC dhidi ya Radio 5 ambapo
Saidi Seif alifunga bao la ushindi kufuatia pasi ya Mohamed Akida
aliyecheza vizuri na Majuto Omary.
Timu
ya netiboli, Taswa Queens ilishinda mchezo wa fainali kwa mabao 19-7,
mchezo ambao ulihudhuliwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.
Taswa
Arusha iliongoza dakika za mwanzoni mwa mchezo kabla ya Taswa Queens
kubadili kibao na kuongoza kwa 10-5 mpaka mapumziko. Sharifa Mustafa,
Veronica Deus na Imani Makongoro walifunga kwa Taswa Queens ambapo
Zuhura Abduknoor, Magreth, Elia, Elizabeth Mbassa, Amina Abdallah,
Rukia Juma, Dosca Munthali alihakikisha Taswa Arusha ambayo ilikuwa
chini ya Rehema Mussa haifurukuti.
Kwa
matokeo hayo, Taswa SC zilitwaa kombe na fedha taslimu Sh 300,000.
Mwenyekiti wa timu hiyo, Majuto Omary aliwapongeza wachezaji wake na
wadhamini, Benki ya TPB, DSTV na Property International Limited kwa
kufanikisha safari hiyo.
Post a Comment