PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: Mbowe Kuelezea Maendeleo ya Tundu Lissu Leo
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe leo Jumanne Oktoba 17, 2017 atazungumzia maendeleo ya afya ya Mb...
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe leo Jumanne Oktoba 17, 2017 atazungumzia maendeleo ya afya ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.

Lissu aliyeshambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi akiwa katika makazi yake Area D mjini Dodoma Septemba 7, amelazwa katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya akiendelea na matibabu.

Akizungumza na Mwananchi Jumatatu, baada ya kuulizwa kuhusu hali ya Lissu, Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni amesema:

“Kesho saa 5:00 asubuhi nitakuwa na mkutano na waandishi wa habari, nitazungumzia hali ya Lissu na mambo mengine yanayoendelea.”

Baadaye katika taarifa ya Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha chama hicho, Tumaini Makene amesema mkutano huo utafanyika makao makuu ya Chadema Kinondoni jijini Dar es Salaam.

“Kupitia Mwenyekiti, Freeman Mbowe chama kitatoa taarifa kwa Taifa kuhusu maendeleo ya Tundu Lissu, mrejesho wa michango, gharama za matibabu,” amesema Makene.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top