Gambo amesema kuwa yeye hana tatizo lolote na Mbunge huyo wa Arusha mjini na kudai kwamba anapaswa kutambua na kubadili aina ya siasa anazofanya kwa kuwa yeye amelenga kutatua matatizo na changamoto za watu wa Arusha Mjini.
"Msuguano na Mbunge haupo lakini anatakiwa tu asome alama za nyakati kwamba Mkuu wa Mkoa wa sasa amedhamiria kuhangaika na shida za watu kama hatalitambua hilo atapoteza muda wake kwa miaka yake yote mitano" alisema Mrisho Gambo.
Aidha Mkuu wa Mkoa huyo amesema kuwa yeye kama kiongozi kijana anahitaji zaidi kukosolewa kuliko kusifiwa ili aweze kujirekebisha sehemu ambayo ana mapungufu ili aweze kuwa kiongozi madhubuti na mahiri zaidi.
Post a Comment