Mapya yaibuka familia ya Lissu na BungeWakati Mbunge wa Singida
Mashariki, Tundu Lissu akiendelea na matibabu katika Hospitali ya
Nairobi, familia yake imefanya kikao cha siri na uongozi ya Bunge
kujadili matibabu ya mbunge huyo.
Kikao hicho kimefanyika leo Jumatatu jijini Dar es Salaam na imeelezwa
kimehudhuriwa na Spika Job Ndugai, Naibu Spika, Dk Tulia Ackson, Katibu
wa Bunge, Thomas Kashilila, Mbunge wa Vunjo, James Mbatia, Mbunge wa
Hanang’, Dk Mary Nagu na ndugu watatu wa Lissu, wanaume wawili na
mwanamke mmoja.
Baada ya kupata taarifa za uwepo wa kikao hicho Mwananchi iliweka kambi
nje ya Ofisi Ndogo za Bunge tangu saa 3:55 asubuhi na kushuhudia
shughuli za kawaida zikiendelea huku kukiwa na watu wachache wanaoingia
na kutoka ndani ya ofisi hizo.
Ilipofika saa 7:40 mchana, alitoka Mbatia akielekea kwenye gari lake
baada ya kumaliza kikao hicho. Mwandishi alimfuata kujua kilichojiri
ndani ya kikao hicho, Mbatia alikiri kuwepo kwa kikao hicho lakini
hakutaka kuzungumza lolote na kuelekeza aulizwe Spika Ndugai.
“Ni kweli tulikuwa kwenye kikao na familia ya Lissu, lakini siwezi
kusema tumezungumzia nini. Kwa taarifa zaidi nendeni kwa Spika au
Katibu wa Bunge, walikuwepo pia ndugu zake watatu, wafuateni wanaweza
kuwaeleza,” alisema Mbatia.
Msemaji wa familia ya Lissu, Alute Mughwai alipotafutwa alisema kikao
hicho kimefanyika kati ya familia na uongozi wa Bunge kuhusu mambo
yanayomhusu Lissu, hata hivyo alisema hakijakamilika kwa sababu ya
kukosekana kwa upande wa Chadema.
Mughwai alisema kikao hicho kimeahirishwa mpaka wakati mwingine pande
zote zitakapotimia ili kulijadili suala hilo kwa ukamilifu wake. Alisema
Chadema kupitia kwa mwenyekiti wake Freeman Mbowe walipewa mwaliko
lakini hawakuweza kufika.
“Siwezi kukwambia tumezungumzia nini, moja ya masharti tuliyopeana ni
kutokusema hadharani mambo tuliyoyajadili lakini yanamuhusu Lissu. Wote
‘interest’ yetu ni kuona Lissu anapona na kuendelea na majukumu yake
kama kawaida,” alisema Mughwai.
Hata hivyo, jitihada za kumtafuta Spika wa Bunge pamoja na Katibu wa
Bunge zilishindikana baada ya simu zao kuita bila kupokelewa.
Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano, Uenenezi na Mambo ya Nje wa Chadema,
John Mrema alipoulizwa kuhusu kikao hicho amesema taarifa kuhusu kikao
hicho zilipelekwa Ofisi ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na siyo
kwenye chama.
Mapya yaibuka Familia ya Tundu Lissu na Bunge
Title: Mapya yaibuka Familia ya Tundu Lissu na Bunge
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Mapya yaibuka familia ya Lissu na BungeWakati Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu akiendelea na matibabu katika Hospitali ya Nairob...
Post a Comment