|
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari-TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko (kulia) akitoa
maelezo kwa Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), kuhusu
mafuta yanavyopakuliwa kutoka kwenye meli, alipotembelea bandarini hapo ili
kupata maelezo kuhusu mchakato wa kupata mita mpya za kupimia mafuta (Flow
Meters), Jijini Dar es salaam. |
|
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania
(TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko (kushoto) akimuonesha Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia), namna maharamia wa
mafuta walivyoharibu miundombinu ya bomba la mafuta baharini, baada ya
kufanikiwa kukamata boti moja na vifaa vyake lililokuwa likitumiwa na wahalifu hao kuiba mafuta. |
|
Boti Jeupe
lililonaswa na kikosi maalumu cha kuzuia uhalifu cha Mamlaka ya Usimamizi wa
Bandari (TPA) juzi wakati wahalifu wakijiandaa kutoboa bomba na kuiba mafuta
kwenye kina kirefu cha Bahari ya Hindi. Wahalifu walifanikiwa kutokomea kusikojulikana
baada ya kujitosa baharini, Dar es Salaam. |
|
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb),
akiwapongeza askari wa doria waliofanikisha kukamata boti moja pamoja na vifaa
vyake muhimu ikiwemo injini baada ya kuwadhibiti maharamia waliotaka kutoboa
bomba na kuiba mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam. |
|
Mmoja wa maafisa wa TPA walioongoza zoezi la
kupambana na wahalifu wanaoiba mafuta kwenye bomba la mafuta akionesha vilipuzi
vilivyokamatwa vilivyokuwa vitumiwe na wahalifu waliokuwa wakijaribu kuiba
mafuta kwenye bomba la mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam |
|
Waziri wa Fedha na
Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akiangalia baadhi ya vifaa ikiwemo
injini ya boti, vilivyokamatwa baada ya wahalifu kukurupushwa baharini
wakijaribu kuiba mafuta kwa kutoboa bomba baharini. |
|
Waziri wa Fedha na
Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kulia)na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko (kulia) na wengine, walipotembela
Bandari ya Dar es Salaam, kitengo cha Mafuta, kukagua flow meters na tukio la
kukamatwa kwa boti lililokuwa likitumika kuhujumu bomba la mafuta. |
|
Waziri wa Fedha na
Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (katikati), akiwa juu ya mitambo ya
kupitisha mafuta kutoka kwenye Meli alipokuwa akipata maelezo ya namna Mamlaka ya
Usimamizi wa Bandari, inavyodhibiti mafuta ili Serikali ipate kodi yake
stahiki. |
|
Waziri wa Fedha na
Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (mbele), akiwa ametoka kukagua mitambo ya kupitisha
mafuta kutoka kwenye Meli ili kujihakikishia kama hakuna namna ya ubadhilifu au
hujuma kwa mapato ambayo Serikali inatakiwa kuyapata |
|
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari
Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit
Kakoko, akitoa maelezo walipokuwa wakiagana na Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb)
|
Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya
Usimamizi wa Bandari (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko, ameiomba Serikali
kuipatia Mamlaka yake vitendeakazi muhimu ili kukabiliana na vitendo vya
uharamia wa bomba la mafuta katika bahari ya Hindi.
Mhandisi Kakoko ametoa maombi hayo
kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, aliyetembelea bandari hiyo
upande wa mafuta na kuelezwa kuhusu tukio lililotokea juzi ambapo TPA
wamekamata boti moja lilikuwa likitumiwa na wahalifu kuiba mafuta kutoka kwenye
bomba, baharini.
Katika tukio hilo watu wasio
fahamika, wakiwa na mabomu na baadhi ya vilipuzi, walilitelekeza boti lao na
kutoweka kusikojulikana kwa kupigambizi baharini baada ya walinzi wa doria
kuwakurupusha kwa kurusha risasi hewani.
“Tunaomba tupatiwe vitendeakazi kwa
ajili ya kikosi chetu kinachofanyakazi kubwa ya kupambana na uhalifu mbalimbali
bandarini hasa magari ili kukiwezesha kikosi hicho kufanyakazi yake kwa ufanisi”
alieleza Bw. Kakoko
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.
Philip Mpango, ameahidi kuipatia Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari vitendeakazi
ambavyo viko ndani ya uwezo wake kama Waziri ili kuongeza udhibiti wa eneo la
maji ya bahari lenye bomba la mafuta.
“Ninawapongenza sana kwa kufanikisha
kuwadhibiti maharamia hao ambao wamekuwa wakitumika kuharibu miundombinu ya
bomba na mafuta na kuharibu mita za kupimia mafuta, nawaahidi kuwatimizia
maombi yenu ya vifaa ambavyo viko ndani ya uwezo wangu” alisema Dkt Mpango’
Alisema kuwa vitendo vinavyofanywa na
wahalifu hao vinakwamisha juhudi za Serikali za kuimarisha miundombinu yake na kusabisha
hasara kwa wenye mafuta na kuikosesha Serikali mapato kutokana na vitendo hivyo
vya kutoboa bomba na kuiba mafuta.
Mbali na kushuhudia boti
lililokamatwa pamoja na vifaa vyake ikiwemo injini na magaloni ya mafuta, Dkt,
Mpango alipewa maelezo kuhusu mchakato unaoendelea wa kufunga mita mpya za
kupimia mafuta (flow meters).
Mhandisi Kakoko ameeleza kuwa
mchakato unaendelea vizuri na kwamba huenda ukakamilika mapema mwakani hatua
itakayosaidia kuongeza mapato ya Serikali bandarini hapo.
Post a Comment