Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Mh Joshua Nasari amesema
yuko tayari kupeleka ushahidi mbele ya Raisi Dkt John Magufuli unaohusu baadhi
ya madiwani waliojiuzulu Chadema na kujiunga na CCM kwamba walipewa rushwa
kushawishiwa kuachia nafasi zao.
Akizungumza leo katika mkutano na wandishi wa habari uliofanyika
kwenye ofisi za chama hicho wilaya ya Arusha mjini,Nasari amesema wakati wowote
kuanzia sasa yupo tayari kuweka ubunge wake rehani endapo ushahidi atakaoutoa
mbele ya raisi utathibitika kuwa uongo kuhusu madiwani hao.
Amesema ushahidi kwamba baadhi ya madiwani hao wamepewa
rushwa umekusanywa na kifaa maalum cha kielectonik Kutoka nchini uingereza
alipokuwa masomoni.
Akizungumzia kuhusu suala la uchomaji wa shule katika
baadhi ya maeneo ya Arusha yaliyotokea mwaka jana Nasari amesema kuwa uchunguzi
alioufanya kupitia amegundua miongoni mwao wapo baadhi ya wateule wa raisi
ambao wanatuhumiana kwamba wanahusika.
Kwa upande wake Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema
amemuomba raisi akubali ushahidi huo na uwekwe hadharani kama ilivyofanyika kwa
ripoti ya Ugunduzi wa wizi wa makinikia .
Haya yanajiri wakati jana baadhi ya madiwani wa chadema
kukihama chama hicho na kuhamia chama cha mapinduzi ccm wakidai kumuunga raisi
katika utendaji wake kwenye mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi.
Post a Comment