PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: Ndugai: Lissu Awezi Kutibiwa Kwa Kuchangishana Michango
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
  Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amefunguka na kudai matibabu ya Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu hayawezi kufanyika...
Ndugai: Lissu Awezi Kutibiwa Kwa Kuchangishana
Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amefunguka na kudai matibabu ya Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu hayawezi kufanyika kwa kuchangishana michango kwa kuwa ana bima yake na haki zake ndani ya Bunge.

Spika Ndugai ameeleza hayo leo asubuhi wakati akizungumza kwenye kipindi cha EA BreakFast kutoka East Afrika baada ya kuulizwa swali kwamba kuna utaratibu gani endapo mbunge akiumia ama akiumwa akiwa kazini.

"Utaratibu ni kwamba wabunge wote wana bima pamoja na mimi mwenyewe, Mawaziri wote wana bima ndani ya bunge kwa sababu ni wabunge kwanza kabla ya kuwa Mawaziri. Kwa hiyo bima zao ndiyo zinazo wahudumia na tuna hudumiwa kupitia hospitali serikali, tunalazwa kama watanzania wengine wowote wale. Ikitokea yanahitajika matibabu ya nje, yatatoka mapendekezo kule Muhimbili kwamba matibabu yake yanapaswa yakitibiwe nje kwa sababu ya upungufu wa jambo fulani hapa nchini", amesema Spika Ndugai.

Pamoja na hayo, Spika Ndugai aliendelea kwa kusema "Tukirudi kwa Mhe. Lissu ni kwamba tulikuwa wote hapa Dodoma, baada ya kuombwa na familia pamoja na Mhe. Mbowe kwamba ni vyema apelekwe kutibiwa hospitali ya Nairobi nchini Kenya tulikubaliana basi ni vizuri aende huko. Lakini alienda huko kama vile ni hospitali binafsi, nje kidogo ya mkondo ule wa kawaida. Kwa hiyo bado bima yake ipo hapa bungeni na utaratibu wa kumtibu upo".

Aidha, Spika Ndugai amesema bunge kwa ujumla haliwezi kumtupa Mhe. Lissu hata kidogo kuhusiana na masuala ya matibabu yake.

"Sisi kama bunge hatujamtupa mwenzetu na bahati nzuri serikali imetoa tamko halijamtupa ni suala la kuwekana sawa, badala ya matamko kwenye vyombo vya habari, magazeti ambayo yamekuwa yakipotosha tu na kuleta malumbano ambayo hayana sababu. Kwa hiyo wito wangu kwa nafasi zote zinazohusika ikiwa ni pamoja na familia ya Lissu, CHADEMA, uongozi wa bunge na serikali endapo tukikaa pamoja hakuna ambacho kitashindwa kuzungumzika, hatuwezi kumtibu mwenzetu kwa michango ya kuchangishana wakati ana bima yake na haki zake", amesisitiza Spika Ndugai.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top