Vita
dhidi ya ujangili katika eneo la ikolojia ya Tarangire na Manyara,
imeongezwa nguvu baada ya Askari wa Shirika la hifadhi za Taifa(TANAPA),
kuanza kushirikiana na Taasisi ya Chemchem foundation na askari wa
jumuiya ya wanyamapori (WMA) ya Burunge kuendesha doria za mara kwa mara
kupambana na majangili.
Katika maeneo ya nje ya hifadhi tayari vitendo vya ujangili vilianza hasa kwa kuuwa wanyama kwa ajili ya vitoweo, ukataji miti kwa ajili ya kuchoma mkaa na uvuvi haramu
Meneja rasilimali watu wa hoteli za Chemchem, Luteni kanali mstaafu, Leonard Werema alisema wameamua kushirikiana ili kuhakikisha eneo lote la ikolojia ya Tarangire- Manyara linabaki salama.
"Hivi
sasa kuna wanyama wengi wapo nje ya maeneo ya hifadhi hasa katika eneo
la Burunge WMA sasa tumeona ni vyema kushirikiana kuhakikisha wanyama
hawa wanakuwa salama ndani ya hifadhi na nje ya hifadhi"alisema
Alisema
kutokana na kuimarishwa kwa ulinzi nje ya hifadhi, hivi sasa wanyama
kama Simba wameanza kuonekana katika eneo la Burunge WMA na wanyama
wengine hatua ambayo inatokana na kuimarishwa uhifadhi na ulinzi.
Meneja
uhusiano wa TANAPA, Pascal Shelutete akizungumza mikakati ya kupambana
na ujangili, alisema jukumu la kulinda wanyamapori na rasilimali za
taifa ni la watanzania wote na akatoa wito wananchi wanaoishi jirani na
hifadhi kusaidia vita dhidi ya ujangili.
"tunawaomba
wananchi kutupa taarifa za watu wanaojihusisha na ujangili watowe
taarifa katika vyombo vya serikali bila ya hofu na serikali itachukuwa
hatua"alisemaMwenyekiti wa Burunge WMA, Ramadhani Ismail inayoundwa na vijiji 10 wilayani Babati mkoa wa Manyara,alisema wamejipanga kuhakikisha majangili wanadhibitiwa katika eneo la Ikolojia ya Tarangire na Manyara.
" katika eneo la WMA vijiji vinanufaika na fedha kutoka kwa wawekezaji ambao ni Un Lodge en Afrika wanaomiliki hoteli za Chem chem,EBN Hunting Safaris,Maromboi Campsite, Burunge Camp site hivyo lazima tunashiriki ulinzi kuhakikisha eneo hili tunalilinda"alisema.
Post a Comment