Diwani wa
kata ya Nkoanekoli Wilson Nanyaro akifafanua jambo katika baraza la madiwani
wa halmashauri ya Wilaya ya Meru .Picha na Ferdinand Shayo
|
Diwani kata ya Malula na Makamu
Mwenyekiti wa Baraza la Halmashauri ya
Wilaya Meru Nelson Mafie akizungumza katika kikao cha Baraza hilo. Picha na Ferdinand Shayo
|
Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Wananchi wa
Vijiji na Kata zinazopakana na hifadhi ya taifa ya Arusha (ANAPA) wameiomba
serikali kupitia kitengo cha Maliasili kuwalipa inayotokana na uharibifu wa mazao ya chakula unaofanywa na
wanyamapori.
Wakiwasilisha
malalamiko kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Meru , Diwani wa kata ya Nkoanekoli Wilson Nanyaro alisema kuwa jumla ya ekari 6 za mazao
zimeharibiwa na wanyamapori hivyo wameiomba idara ya Maliasili ili kunusuru
kaya 12 na uhaba wa chakula.
Nanyaro
alisema kuwa katika kipindi hiki cha mavuno wananchi hao wamepata mazao
machache sana kutokana na mazao yao kuliwa na nyani ambao hutoka hifadhi hiyo
ya taifa.
Diwani viti
Maalumu kata ya Embaseny Agness Lambo Alisema kuwa wamekua wakitoa taarifa kwa
idara hiyo ila wakichelewa kuzifanyia kazi kwa muda muafaka hivyo kusababisha
maumivu ya kiuchumi kwa wananchi ambao hutegemea kilimo kujikwamua kimaisha.
“Wananchi
waliokubwa na adha hii wanaishi umbali mrefu kutoka katika hifadhi ya Arusha tumekua
tukitoa taarifa ila Maafisa wa Maliasili wamekua wakichelewa mara kwa mara
hivyo kusababisha wananchi kutokupata haki stahiki” Alisema Lambo
Afisa
Maliasili Halmashauri ya Wilaya ya Meru Bernad Saruni amekiri kuwepo kwa
tattizo hilo na tayari wameanza kuwalipa fidia wananchi wa kijiji cha
Leguruki,Ngarinanyuki fedha ambazo ni
kifuta machozi baada ya uharibifu huo kutokea.
Post a Comment