Mkurugenzi wa
Kampuni ya Candy& Candy, Josiah Kiman Kairuki(38), Mkazi wa
Mikwecheni Jijini Dar es Salaam juzi alipandishwa tena Kizimbani, katika
mahakama ya hakimu mfawidhi wilaya ya Longido, mkoa wa Arusha, kujibu
tuhuma za kujipatia kiasi cha sh 336 milioni kwa njia ya udanganyifu,
baada ya kudai kuwa ana kontena la simu za I Phone 7 limezuiwa katika bandari ya Dar es Salaam.
Kairuki
ambaye ni Raia wa Kenya , Julai 26 mwaka huu, mahakama ya hakimu
mfawidhi wa wilaya ya Longido, ilimwachia huru katika shitaka hilo la
kujipatia fedha hizo kwa njia ya udanganyifu, kutoka kwa Yusuph
Mohamed kutokana na maombi ya Jamuhuri yaliyowasilishwa mahakamani na
Mwendesha mashitaka, Mkaguzi wa polisi Anastazia Mutatina.
Hata
hivyo Kairuki, baada ya kuachiwa huru na Hakimu mfawidhi wa mahakama
hiyo, Aziza Temu, alikamatwa na polisi akiwa nje ya mlango wa mahakamani
na kurejeshwa kituo cha polisi cha wilaya ya Longido kwa mahojiano
zaidi.
Kuf ikishwa tena mahakamani.
Mkurugenzi
huyo juzi, aliunganishwa na Abdinasiri Adamnuru na mbele wa hakimu
mfawidhi wa wilaya ya Longido, Aziza Temu, walisomewa mashitaka mawili
kujipatia fedha hizo kwa njia ya udanganyifu na kosa la pili lilimuhusu
Adamnuru kujifanya afisa forodha Tanzania.
Mwendesha mashitaka, Mkaguzi wa polisi Anastazia Mutatina alisema, watuhumiwa hao, walifanya makosa hayo, kati ya Januari 23 na june 10, 2017 na upelelezi wa shitaka hilo bado haujakamilika.
Hata
hivyo, aliomba watuhumiwa hao, wasipewe dhamana kutokana na kiasi
kikubwa cha fedha wanachotuhumiwa na pia wote kutokuwa na makazi wa
kudumu.
Hakimu
Temu alikubali maombi ya upande wa mashitaka na watuhumiwa hao,
walirejeshwa katika mahabusu ya Kisongo Arusha hadi August 23 mwaka huu
kesi yao itakapotajwa tena.
Post a Comment