Na Mwene Said wa Blogu ya Jamii, Dar es Salaam.
Mahakama
Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, imeupa muda wa siku tano
kuwasilisha pingamizi la awali dhidi ya maombi ya dhamana ya kesi ya
uhujumu uchumi inayomkabili Mfanyabiashara Yusufali Manji (41) na
wenzake watatu.
Manji
na wenzake, pia wanakabiliwa na kukutwa na vitambaa vya sare za Jeshi
la Wananchi Tanzania (JWTZ) isivyo halali vyote vikiwa na thamani ya
Sh. milioni 236.5.
Hata
hivyo, mfanyabiashara huyo amefungua maombi yaliyosajiliwa kwa namba
122/2017, kupinga hati iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini
(DPP) kuzuia dhamana dhidi yake na yalitajwa jana mbele ya Jaji Isaya
Arufani.
Upande
wa mashtaka ukiongozwa na Paul Kadushi, Simon Wankyo na Tulumanywa
Majigo, ulidai mahakamani kwamba wanaomba muda kwa sababu wana nia ya
kuwasilisha pingamizi la kupinga maombi ya utetezi.
Pia, ulidai kuwa wanaomba mahakama iwape muda wa kuwasilisha majibu ya hati ya maombi ya mshtakiwa.
Jaji
Arufani alisema upande wa Jamhuri uwasilishe majibu na pingamizi lao
Agosti Mosi na upande wa utetezi kama watakuwa na majibu ya nyongeza
wawasilishe Agosti 2 na mahakama hiyo itasikiliza maombi hayo Agosti 4,
mwaka huu.
Katika
maombi hayo, Manji anaiomba Mahakama Kuu kutengua hati ya DPP ya
kuzuia dhamana yake iliyowasilishwa Julai 5, mwaka huu aliposomewa
mashtaka ya uhujumu uchumi ikiwamo kukutwa na sare hizo.
Aidha, anaiomba mahakama iridhie kumpa dhamana kwa sababu ana matatizo ya kiafya.
Kwa
mujibu wa hati ya maombi hayo, Manji anadai kuwa anasumbuliwa na
maradhi ya moyo na kwamba ameambatanisha vyeti vya daktari katika
maombi yake.
Katika
kesi ya msingi, Manji na wenzake wanatuhumiwa kukutwa na mihuri ya
mbalimbali ya JWTZ isilivyo halali vyote vikiwa na thamani ya Sh.
milioni 236.5.
Mbali
na Manji, washtakiwa wengine ni, Ofisa Rasilimaliwatu Deogratias
Kisinda (28), Mtunza Stoo, Abdallah Sangey (46) na Mtunza Stoo msaidizi,
Thobias Fwele (430
Ilidaiwa
katika shtaka la kwanza kuwa Juni 30, mwaka huu eneo la Chang'ombe
Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam, Manji na wenzake walikutwa na
askari polisi wakiwa na Mabunda (majola) 35 ya vitambaa vya
vinavyotengezea sare za JWTZ zenye thamani ya Sh. milioni 192.5 na
kwamba zilipztikana isivyo halali.
Katika
shtaka la pili, ilidaiwa kuwa mekutwa Julai Mosi, mwaka huu eneo la
Chang'ombe 'A' Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam, washtakiwa wote
kwa pamoja walikutwa na askari polisi wakiwa na mabando nane ya sare za
JWTZ zenye thamani ya Sh. milioni 44.
Upande
huo wa Jamhuri uliendelea kudai kuwa, Juni 30,mwaka huu eneo la tukio
la kwanza, washtakiwa walikutwa na mhuri wa JWTZ uliokuwa na maandishi
'Mkuu wa Kikosi 121 Kikosi cha Jeshi JWTZ' bila kuwa na uhalali kitendo
ambacho kinahatarisha usalama wa nchi.
Majigo
aliendela kudai katika shtaka la nne, siku ya tukio la tatu, washtakiwa
wote kwa pamoja walikuwa na mhuri wenye maandishi "Kamanda Kikosi 834
Kj Makutupora Dodoma" bila uhalali kitendo ambacho kinahatarisha usalama
wa nchi.
Shtaka
la tano, siku ya tukio la tatu na la nne, mshtakiwa alikutwa na mhuri
wenye maandishi "Comanding Officer 835 Kj Mgambo P.O BOX 224 Korogwe"
bila kuwa na uhalali kitendo ambacho kinahatarisha uslama wa nchi.
Ilidaiwa
katika shtaka la sita, Julai Mosi, mwaka huu eneo la Chang'ombe 'A',
washtakiwa wote walikutwa na pleti namba za gari zenye usajili wa SU 383
iliyopatikana isivyo halali.
Majigo
alidai katika shtaka la saba, eneo la tukio la sita, washtakiwa
walikutwa na pleti namba za gari zenye namba ya usajili SM 8573
iliyopatikana isivyo halali.
Kwa
mujibu wa mashtaka hayo yaliyofunguliwa chini ya sheria ya uhujumu
uchumi na usalama wa taifa, washtakiwa hawakutakiwa kujibu chochote kwa
sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi yao.
Upande
wa Jamhuri uliwasilisha hati ya kuzuia dhamana kutoka kwa Mkurugenzi wa
Mashtaka Nchini (DPP), akiomba washtakiwa wasipewe dhamana kwa usalama
wao na maslahi ya taifa.
Pia, DPP alieleza sababu nyingine kwamba mahakama hiyo haina mamlaka ya kushughulikia dhamana dhidi ya kesi hiyo.
Kesi ya msingi pia itatajwa Agosti 4, mwaka huu katika Mahakama ya Kisutu.
Post a Comment