Waziri
wa Nchi - Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene (kulia)
akizungumza na wananchi baada ya kupokea malalamiko yao katika Kijiji
cha Lukole kuhusu shida ya maji wanayoipata, wakati alipokwenda kwenye
bomba la Kijiji kuzungumza na wakinamama ambao ndio waathirika wakubwa
wa tatizo hilo na kuwataarifu namna ambavyo amekwishaanza kushughulikia
kero hiyo.
Na Nteghenjwa Hosseah - Kibakwe.
Uharibifu
wa vyanzo vya maji ni tatizo lililokithiri katika maeneo mengi Nchini
Tanzania huku wananchi wa maeneo hayo wakiendelea kushuhudia na
kuvumilia uharibifu huo eti kwa sababu tu wahusika ni ndugu, jamaa ama
marafiki wa jamii husika.
Pasipo
kujali athari zinazoweza kutokea kutokana na uharibifu wa mazingira
hususan vyanzo vya maji wananchi wameendelea kulima, kufuga, kuchunga
pamoja na kuishi katika maeneo hayo pasipo kuwa na shaka yoyote na
kusababisha ukosefu wa maji kwa jamii inayotegemea vyanzo hivyo.
Athari
zaidi zimethibitija katika Kijiji cha Chinyika na Lukole vilovyopo
kata ya Chinyika kwa kukosa maji kutokana na Uharibifu uliofanywa na
baadhi wa wananchi katika chanzo cha maji kwenye milima ya wota ambacho
ndio chanzo kikuu cha maji ya mtiririko kwa wananchi zaidi ya elfu saba.
Waziri
wa Nchi - Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene (katikati
aliyekaa) akisimikwa kuwa Chifu wa Kigogo katika Mkutano wa hadhara
uliofanyika katika Kijiji cha Kingiti.
Hali
hii imepelekea wananchi wa vijiji hivyo vyenye vitongoji zaidi ya kumi
na tano kuwekeana zamu ya kuchota maji ambapo kwa wiki kila Kijiji
hupata maji kwa siku tatu na kila kaya huchota Ndoo nne kwa siku ya zamu
yao ambapo kiasi hicho hakiwajawahi kuwatosha mahitaji ya Kaya.
Wananchi
wa Kijiji cha Chinyika wamepaza sauti zao kwa Waziri wa Nchi - Ofisi ya
Rais (Tamisemi), George Simbachawene wakati wa ziara yake katika
vijiji hivyo na kulalamikia tatizo la upungufu wa maji na adha
wanayopata kutokana na hali hiyo.
Waziri
Simbachawene ameshuhudia foleni ndefu ya ndoo za wakinana wakiwa
bondani kusubiria kupata japo maji ya kupikia chakula cha Familia,
Wakinamama hao hushinda zaidi ya siku nzima bombani hapo au pengine
kukesha ili kuwa na uhakika wa kupata japo ndoo moja ya maji kwa
matumizi ya nyumbani.
Akizungumza
na wakinamama Waziri Simbachawene amesema anatambua adha wanayoipata na
amewahakikishia kwamba ataanza kutatua changamoto hiyo kwa kuhakikisha
wale wote wanaharibu vyanzo vya maji katika Wilaya ya Mpwapwa wanatiwa
nguvuni na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Waziri
wa Nchi - Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene akizungumza na
wananchi wa Kijiji cha Kingiti wakati wa zaiara yake katika Jimbo la
Kibakwe.
“Ninajua
kwamba waharibifu wa vyanzo hivi ni watu wenye nguvu lakini na mimi
ntaongeza nguvu kwenye Kikosi kazi cha Wilaya ili kuhakikisha kwamba
wale wote wanaoishi karibu na vyanzo hivyo wanahamishwa na mazao yao
yanaharibiwa, mifugo inaondolewa na wanapelekwa Mahakamani” alisema Mhe.
Simbachawene.
Pia
aliongeza kuwa Fedha zimekwishatengwa zaidi ya Tsh Mil 160 kwa ajili ya
ukarabati ya miundombinu inayotoa maji kutoka katika Milima ya Wota
kupitia Kingiti hadi kufika Lukole na Halmashauri ya Mpwapwa imeanza
utekelezaji wa mradi huu utakaokuwa na manufaa kwa wananchi na ataongeza
Tsh Mil 13 kwa ajili ya kuchimba kisima.
Naye
Mhandishi wa Maji katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, Apolonia
Temu ameelezea sababu ya ukosefu wa maji katika vijiji hivyo kuwa ni
pamoja na uharibifu wa mazingira, ongezeko la watu ukilinganisha na hapo
awali na uchakavu wa miundombinu ambayo kwa sasa imeanza kukarabatiwa.
Waziri
Simbachawene ameendelea na ziara yake katika Jimbo la Kibakwe na kwa
siku ya tatu ametembelea vijiji vya Lukole, Kingiti na Itenge ambapo
amefanya mikutano ya hadhara, amesikiliza kero za wananchi pamja na
kukagua miradi ya maendeleo.
Post a Comment