Mtuhumiwa huyo alipokuwa akishuka katika gari la magereza na kuingizwa mahakamani kusikiliza kesi yake |
akisindikizwa na askari magereza kuingia chumba cha mahakama |
Mtuhumiwa huyo ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya Candy &Candy alipofikishwa mahakamani hap |
Mwandishi
Wetu,PMT
Kairuki ambaye ni Raia wa Kenya , anatuhumiwa
kujipatia kiasi cha sh 336 milioni kwa udanganyifu kutoka kwa Yusuph Mohamed
ili akombowe kontena hilo katika bandari ya Dar es Salaam, kitu ambacho ni uongo.
Mwendesha mashitaka wa polisi,Anzelini Muhela,
alieleza mahakamani, mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Longido,Aziza Temu kuwa
mtuhumiwa huyo amejipatia fedha hizo kati ya Januari 23 na june 10, 2017.
Mwendesha mashitaka
alisema upelelezi wa shauri hilo, haujakamilika na aliomba mtuhumiwa huyo
asipewe dhamana kwani,uraia wake una utata akiwa
nje anaweza kusababisha kupotea kwa nyaraka za kesi na kiasi alichojipatia ni
kikubwa na akiwa dhamana anaweza kutoweka.
Hata hivyo, Wakili wa Kairuki, John Mallya alipinga
hoja zote za mwendesha mashitaka na kueleza dhamana ni haki ya kikatiba ya
mtuhumiwa ambaye bado hajatia hatiani.
Mallya alisema pia maombi hayo ya jamuhuri,
yalitakiwa kuwasilishwa chini ya kiapo kwa mujibu wa mwenendo wa makosa ya
jinai sura 396(A) kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2011.
Hakimu Temu aliahirisha kesi hiyo, hadi julai 26 mwaka
huu, ambapo atatoa maamuzi ya kumpa dhamana mtuhumiwa huyo ama kutompa.
Post a Comment