PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: Wenger Apewa Paun Milioni 165 za Usajili..Aambiwa Msimu Ujao Ubinga Utue Emirates Stadium..!!!
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
  Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger ambaye anafahamika kwa ubahili, amepewa kitita kikubwa cha fedha akiambiwa azitum...



Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger ambaye anafahamika kwa ubahili, amepewa kitita kikubwa cha fedha akiambiwa azitumie kufanya usajili wa wachezaji wapya.

Mabosi wa klabu hiyo wamemtengea kocha huyo Mfaransa Pauni 165 milioni na kumweleza azitumie kuimarisha kikosi chake.

Bodi ya klabu hiyo imempa kitita hicho kikubwa cha fedha ili kumwezesha kushindana na wababe wengine England kwenye soko la usajili.

Tayari, Wenger anayo majina ya Riyad Mahrez wa Leicester City na Mturuki Arda Turan ambaye ameachwa na Barcelona.

Wenger ameambiwa awe makini na kikosi chake Arsenal msimu ujao kwani mwisho wa msimu atatakiwa kutwaa taji ambalo amelikosa tangu msimu wa 2004.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top