PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: Full Ripoti: Daktari Afichua Mume wa Zari alipewa Sumu
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
KAMPALA: Imefichuka! Nyuma ya msiba ulioacha historia wa aliyekuwa mzazi mwenza wa staa wa Afrika Mashariki, Zarinah Hassan ‘Zari The ...
KAMPALA: Imefichuka! Nyuma ya msiba ulioacha historia wa aliyekuwa mzazi mwenza wa staa wa Afrika Mashariki, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, Ivan Ssemwanga ‘The Don’ aliyepatwa na umauti wiki iliyopita akiwa amelazwa kwenye Hospitali ya Steve Biko, Pretoria nchini Afrika Kusini, kuna mengi yanayosemwa, Wikienda liko bega kwa bega na kinachojiri.
Miongoni mwa yanayosemwa ni madai ya jamaa huyo kupewa sumu iliyomdhuru moyo hivyo kusababisha kifo chake.

MADAI YA SUMU

Chanzo cha ndani ya familia ya Ivan kililieleza gazeti moja maarufu nchini Uganda kuwa, Ivan alilishwa sumu na watu ambao hawakuwataja na kwamba mara ya mwisho alikuwa akipata chakula na ndugu zake kabla ya hali yake kuanza kuwa mbaya kisha siku chache baadaye alikimbizwa katika Hospitali ya Steve Biko.

Gazeti hilo lilimkariri mtu huyo akieleza kuwa, Ivan hakufa kwa shambulio la moyo wala moyo kushindwa kufanya kazi bali aliwekewa sumu kali kwenye chakula.

MAUMIVU MAKALI

Sosi huyo alisema kuwa, baada ya sumu hiyo, muda mwingi Ivan alikuwa akilalamika maumivu makali ya tumbo na kuomba kuwahishwa hospitalini.

Hata hivyo, mbali na madai hayo, taarifa za kitabibu zilieleza kuwa, Ivan alifariki dunia kutokana na shambulio la moyo bila kuweka bayana kama alipewa sumu au la.

Katikati ya mkanganyiko huo, Wikienda lilizungumza na daktari wake aliyekubaliana na maelezo kuwa inawezekana sumu hiyo ndiyo iliyomdhuru moyo na kumsababishia tatizo la Atrial Fibrillation.

ATRIAL FIBRILLATION NI NINI?

Daktari huyo alisema kuwa, Atrial Fibrillatoni ni ugonjwa ambao huufanya moyo badala ya kuwa unadunda kama ilivyo kawaida, uwe unatetemeka na kusababisha shida katika mfumo mzima wa upumuaji na usukumaji wa damu.

“Tatizo hili, huwa linatokea kwenye chemba za juu za moyo (Atria) ambazo kimsingi misuli yake ndiyo inayosababisha moyo kudunda.

“Misuli hii inapoishiwa nguvu, hushindwa kuzalisha nguvu ya kutosha kusukuma damu na badala yake, hutetemeka na matokeo yake, damu huanza kuganda kwenye mishipa (blood clotting) kwa sababu ya kukosekana kwa presha ya kuisukuma na kuifanya izunguke mwili mzima kisha kurudi tena kwenye moyo.

“Kwa baadhi ya watu, tatizo hili hutokea mara moja na kuacha au kwa kitaalam Sporadic Fibrillation na kwa wengine, ikitokea mara moja huendelea bila kupata ahueni yoyote au kwa kitaalam Persistent Fibrillation.

NINI CHA KUFANYA?

“Unapoona hali ya aina hiyo ni muhimu kuwahi hospitalini baada ya kuona dalili za ugonjwa huu kwani ukichelewa, husababisha damu kuganda kwenye viungo muhimu katika mwili, hasa kwenye ubongo.

“Pia inapotokea damu imeganda kwenye ubongo, husababisha mifumo mingine ya mwili kama upumuaji na mfumo wa fahamu kuwa kwenye hatari ya kushindwa kufanya kazi, jambo ambalo ni hatari kwa maisha.

“Inapotokea damu imegandia kwenye ubongo kutokana na tatizo hili, madaktari ni lazima wafanye kwanza upasuaji wa kuondoa damu hiyo kwenye ubongo kisha baada ya hapo ndipo waendelee na kutibu chanzo cha tatizo, ambacho huwa ni kwenye moyo.


“Mara zote, Atrial Fibrillation husababisha mgonjwa apatwe na ‘stroke’ na endapo tatizo hili likiwa ni lile la kuendelea, Persistent Fibrillation, uwezekano wa mgonjwa kupona huwa mdogo.

NINI KINASABABISHA?

“Yapo mambo mbalimbali yanayoweza kusababisha tatizo la Atrial Fibrillation, miongoni mwa hayo ni matatizo ya shinikizo la damu ya muda mrefu, kuziba kwa mishipa ya damu kunakoweza kusababishwa na mwili kuwa na mafuta mengi (cholesterol). “Hii huwapata zaidi watu wanene. Pia matatizo katika valvu za moyo, huweza kusababisha tatizo hili.

“Atrial fibrillation inaweza pia kusababishwa na kuumia kifua au upasuaji wa kifua ambao haukwenda vizuri. Wapo pia watu waliopatwa na tatizo hili kwa sababu ya kunywa sana pombe kupita kiasi.

UWEZEKANO MDOGO WA KUPONA

“Tiba za muda mrefu huweza kusababisha mgonjwa akapona ingawa nafasi ya kupona kwa wagonjwa wanaopatwa na Persistent Fibrillation huwa ni ndogo,” alisema daktari huyo.

ZARI, MASHEMEJI ZAKE PACHIMBIKA

Hata hivyo, wakati Ivan akiagwa leo nchini Uganda kisha kuzikwa kesho, kuna taarifa zilizoenea mno wikiendi iliyopita zikionesha kuwa, katika kipindi cha kuuguza, Zari alikuwa ‘bize’ akisuguana na kaka wa Ivan pamoja na mashemeji zake akiwemo King Lawrence juu ya mali alizoacha marehemu.

IVAN AMEACHA NINI?

Ivan ameacha shule sita nchini Afrika Kusini, hoteli mbalimbali pamoja na majumba nchini Uganda. Ameacha pia watoto watatu, Pinto, Raphael na Quincy.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top