PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: YANGA YATUA JIJINI ARUSHA KWA KISHINDO HUKU IKIWA NA KOMBE LAKE NA KUPOKELEWA NA MAMIA YA WAPENZI WA SOKA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
 hapa walipokuwa wakitangazwa mabingwa na kukabidhiwa kombe la ubingwa katika uwanja wa CCM KIRUMBA jijini Mwanza Picha mbalimba...


 hapa walipokuwa wakitangazwa mabingwa na kukabidhiwa kombe la ubingwa katika uwanja wa CCM KIRUMBA jijini Mwanza

Picha mbalimbali za mabingwa wa soka Tanzania Dar Young African walipokuwa wakiwasili jijini Arusha wakitokea mjini Dodoma  ambapo walipokelewa na wapenzi wa soka kuanzia maeneo ya meserani na kuungana na msafara mkubwa wa wapenzi wa soka jijini Arusha waliokuwa na kiu ya kushuhudia kombe hilo na timu hiyo itakayocheza leo mchezo wa kirafiki na AFC ya jijini hapa

Kikosi cha Afc Arusha kimejinasibu kuwa kitawafunga mabigwa wa ligi kuu bara msimu uliomalizika  Timu ya  Yanga Afrika,katika mchezo wao wa kirafiki unaotajarajiwa kuchezwa Jumapili hii  May 28 katika kiwanja cha kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid jijini hapa


Akiongea na gazeti hili kocha wa kikosi hichi kipya cha timu ya AFC Fikiri Elias  alisema kuwa vijana wake wapo tayari kuwapatia burudani wapenzi wake wa soka mkoani hapa huku akiwapa sifa viongozi wa serikali kwa kuwa bega kwa bega katika kuhakikisha soka la mkoa wa Arusha linarudi katika ramani yake

Alisema kuwa japo hii ni mechi yao ya kirafiki baina yao na timu ya Yanga lakini watatumia mchezo huu pia kuangalia kikosi bora ambacho kitakaa kambini kwa ajili ya kuandaa timu ya kikosi kitakacho unda AFC mpya itayoshiriki ligi daraja la kwanza .


,, pamoja ya kuwa timu ya yanga inawachezaji wazoefu wengi na pia ndio wametoka tu kutwaa ubigwa mara ya tatu lakini napenda kusema hivi japo mechi hii ni ya kirafiki lakini nimeaada kikosi kizuri na ninauhakika lazima tutaifunga timu hii ili tuweke historia japo ni mechi ya kirafiki ,,alisema Fikiri



Kwa upande wake kocha msaidizi  timu ya  Yanga ambao wameshikilia ubigwa  kwa mara ya tatu mfulul

izo ligi kuu bara  Juma Mwambusi alisema kuwa mchezo huu ni muhimu  kwao kwani ni moja  ya program zao katika kujiandaa kuelekea katika michuzano inayowakabili  ikiwemo mashindano ya Sport Pesa


Kikosi hichi cha yanga kipo katika ziara ya kutembeza kombe lake kwa mashabiki wa mikoani ambapo mkoa wa Arusha umekuwa wa kwanza kuona kombe hilo na wakitoka mkoani hapa wanampango wa kulipeleka mkoani Dodoma ,ambapo pia wanajangwan hawa wamekuwa ni timu ya tatu kuoka ligi kuu bara msimu ulioisha kutoa katika aridhi ya jiji la Arusha iliyokuwa na ukame wa timu za ligi kuu mara baada ya timu za Ruvu shooting na Simba  zilizowaikutua hapa katika mtanange wake ulioisha



Akizungumzia mchezo huo wa kirafiki  mmoja wawaandaaji wa mechi hiyo ambayo katibu wa timu ya AFC  Charles Mwaimu alisema kuwa maandalizi yote yamekamilika timu zote zipo tayari wanaisubiri tu siku ya mechi ifike.



Aliwasihi wananchi wa mkoa wa Arusha na pembezoni kujitokeza kwa wingi kuishabikia timuyao ya AFC ikiwa ni ujio mpya wa timu hii mara baada ya kupotea kwa muda ,na aliwasihi wananchi wa mkoa wa Arusha kujitokeza kuwapa morali wachezaji wao .



Aidha alisema kuwa pia mbali na mechi hii ya yanga kucheza na AFC pia wanampango wa timu hii kwenda mkoani manyara kucheza mechi baida yao na timu ya Mererani.


About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top