Mbunge
wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu ameibuka na kuishauri
serikali jambo la kufanya kutokana na matokeo ya uchunguzi wa mchanga wa
madini uliofanywa na kamati ilyoundwa na Rais John Magufuli.
Tundu
Lissu anasema Tanzania ni mwanachama wa 'The MIGA Convention' hivyo
ukiwa mwanachama ukachukua mali za wawekezaji wao utapelekwa kwenye
mahakama za kimataifa na kwenda kushughulikiwa huko, hivyo Tundu Lissu
ametoa ushauri wa namna nzuri ya kushughulika na watu
"Sisi
Tanzania ni wanachama wa kitu kinaitwa 'The MIGA Convention'
Multilateral Investment Guarantee Agency ya benki ya dunia, ukiwa
mwanachama wawekezaji wakileta mali zao kwako, ukichukua mali zao kama
walivyochukuliwa mali zao namna hii utapelekwa kwenye mahakama zao za
kimataifa unaenda kushughulikiwa huko, tumesaini mkataba wa ulinzi wa
wawekezaji na mataifa wanayotoka wawekezaji hao Marekani, Canada,
Uingereza wote ni mabosi wakubwa makampuni ambayo Rais ameyakamatia mali
zao yanatoka kwenye hizi nchi tuna 'bilateral investment treaties
ambazo zinalinda mikataba hii" alisema Tundu Lissu
Tundu
Lissu anasema hili suala tusipokuwa makini nalo linaweza kuleta
matatizo makubwa huku akimtaja muhusika wa mikataba iliyolifikisha taifa
katika hasara iliyobainika katika uchunguzi huo.
"Rais
anajiingiza kwenye mgogoro mkubwa, akimkamata Dalali Kafumu peke yake,
tutamwambia kwanini siyo Gray Mwakalukwa mikataba yote hii imeingia
wakati wa Mr. Gray Mwakalukwa, kwanini siyo Daniel Yona, kwanini siyo
Jakaya Kikwete sababu alikuwa Waziri na mimi nina mkataba wa Bulyankulu
na kwanini siyo mawaziri wote, kwa sababu mikataba iliingiwa wakiwa
mawaziri" alisema Tundu Lissu
Lakini mbali na kusema yote hayo Tundu Lissu alitoa ushauri wake katika suala hilo...
"Kama
unataka kufanya haya unayoyafanya elewa hali halisi ilivyo, tatizo liko
wapi kama tatizo ni kwamba tunapata mapato kidogo na kweli wanatupiga
kweli kweli ila kama utaka kufanya mambo kweli kweli kajiondoe kwanza
MIGA ili hao wawekezaji wasikushtaki kwenye hizo mahakama za huko, maana
wakikushtaki kule unanyolewa bila maji, hakuna ndege ya Tanzania
itakanyaga hizo nchi wataikamata, hakuna hela tutaweka kwenye nanii za
kimataifa watazikamata, kwa sababu tunavunja mikataba ya kimataifa
inayolindwa na sheria za kiwekezaji za kimataifa, kwa hiyo anzia huko
juu ukimaliza mikataba ya kimataifa, njoo kwenye mikataba kati ya nchi
na nchi ondoa hiyo mikataba ukishaondoa hiyo hushtakiki nje, baada ya
hapo njoo ndani sababu bado unaweza kushtakiwa ndani" alisisitiza Tundu Lissu
Post a Comment