Mbunge wa Kigoma Mjini, Zuberi Zitto Kabwe amesikitishwa na kitendo
kilichofanywa na moja ya askari polisi kumtishia bunduki aliyewahi kuwa
Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima.
Zitto kabwe ameonyesha masikitiko hayo kupitia ukurasa wake wa kijamii
Facebook akihoji kama polisi wanafundishwa kuwafanyia hivyo raia.
"Hii ni nini ?, askari wetu wanafundishwa kufanya hivi, Waziri Mwigulu
huyu yupo wazi na ni wa kutoka kwako. Unahitaji uchunguzi". Ameandika
Zitto
Zitto ameandika hayo baada ya masaa machache kupita kwa tukio hilo
lililowahusisha askari hao walioambatana na kampuni ya Majembe Auction
Mart waliokuwa wakitaka kujaribu kukamata gari iliyokuwa imeegeshwa
pembeni ya barabara ya Masaki karibu na Hoteli ya Double tree ingawa
ndani ya gari hilo alikuwepo dereva.
Post a Comment