Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba bungeni amesema
serikali bado haina sheria ya kuthibiti matumizi ya kilevi aina ya
shisha ila lipo agizo la Waziri Mkuu la kupiga marufuku biashara hiyo na
kutaka agizo hilo lifuatwe na kila mtu.
Mwigulu Nchemba amesema hayo wakati akijibu swali bungeni kuhusu
matumizi ya kilevi hicho cha shisha ambacho bado katika baadhi ya maeneo
kimeendelea kutumika na kuleta athari kwa watumiaji.
"Ni kweli serikali baada ya kuona matumizi ya kilevi cha Shisha yanaleta
athari kwa binadamu, serikali imeanza kuweka sheria za kuthibiti
matumizi ya shisha, usambazaji wa shisha na uagizaji wa kilevi hicho,
lakini wakati tunasubiri sheria hizo tunatambua kuwa lipo agizo la
Waziri Mkuu la kupiga marufuku matumizi ya kilevi cha shisha ambalo
utekelezaji wake ulianza mikoani kama Dar es Salaam, Mbeya, Iringa na
mikoa mingine imeendelea kuitikia. Kwa hiyo maelekezo ya Mh. Waziri Mkuu
yanafanyiwa kazi bila kupunguza hata nukta" alisema Mwigulu Nchemba
Mbali na hilo Waziri Mwigulu alisema anatambua wapo watu walipewa leseni
kwa ajili ya kufanya biashara hiyo ya shisha lakini kwa kuwa serikali
inajali masuala ya afya ya Watanzania ndiyo maana wanatakakuja na sheria
ili kuthibiti kilevi hicho ambacho kina athari kwa watumiaji.
Post a Comment