Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Mohammed Mpinga, amesema mara baada ya kusikia ajali iliyoua wanafunzi zaidi ya 30 wa Shule ya Lucky Vicent ya Mkoani Arusha, alichukua hatua kadhaa na sasa wanafanya operesheni ya nchi nzima.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Mohammed Mpinga.
Akizungumza na kipindi cha Super Mix cha East Afrika Radio, Kamanda Mpinga amesema alipata mshkuko mkubwa sana hasa alipoambiwa lile gari limetumbukia kwenye korongo likiwa na wanafunzi.
“Kitu cha kwanza nilichofanya, kwa vile mimi ni msaidizi wa Inspector General wa Jeshi la Polisi, ilibidi kumtaarifu, sambamba na hilo ni kumuelekeza mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Mkoa wa Arusha kufuatilia kwa ukaribu na kunipa taarifa mara kwa mara.
“Aidha vile vile nikaongea na RPC wa Mkoa wa Arusha kuhusu tukio lile na kutoa maelekezo ya kufuatilia kwa karibu ile kuweza kujua nini hasa chanzo cha ajali,” amesema.
Katika hatua nyinge Kamanda Mpinga amesema kwa sasa wanafanya operesheni ya nchi nzima kwani ajili ile imewafanya waongeze nguvu zaidi.
“Sio kwamba huko nyuma tulikuwa hatufanyi lakini tukio hili sasa limeongeza umakini na kizuri ni kwamba tunaungwa mkono na wakuu wa shule, wamiliki, wananchi kwa ujumla, na wazazi kwamba ni zoezi ambalo tunafanya ni zuri.
“Uko nyuma walikuwa wakilalamika wanafunzi wetu wataendaje shule, lakini sasa tunaungwa mkono, kwa hiyo lazima tufanye kwa nguvu na kila mtu anaona umuhimu wa usalama wa mtoto wake anapokwenda shule na anaporudi,” amesema na kuongeza.
“Bodaboda si sahihi kubeba wanafunzi kwa kupeleka shule lakini tax ni sawa endapo itazingatiwa idadi inayotajwa kwa mujibu wa sheria, yaani nyuma wanafunzi watatu na mbele mmoja, hiyo ni sahii hakuna tatizo. Hata kwenye bajaji si sahihi, lakini mtoto chini ya umri wa miaka tisa huwezi kumpakia kwenye bajaji hadi awe na mtu mwingine mkubwa amekaa naye na si vinginevyo,” amesema Kamanda Mpinga.
Amesema kuwa ukaguzi ambao wanaofanya, kwanza ni uzima wa gari lenyewe, kujua kama linafaa kukaa barabarani, pia ukaguzi kuhakikisha nyaraka zote wanazo, idadi ya wanafunzi wanaopakia ipo sawa sawa na uwezo wa gari lenyewe, pia je wana leseni ya Sumatra ya kupakia wanafunzi, na kama ni gari la wanafunzi linatakiwa kupakwa rangi ya njano na ubavuni kuandikwa School Bus kila mtu ajue lile gari ni la wanafunzi.
“Kibaya ninachosikia hawa wamiliki wa mabasi wameyaficha magari, wanaogopa kuyaleta barabarani lakini tunachotaka kufanya tuende mpaka kwenye shule zenyewe tukute magari kule. Watu wanafikiri hadi kitu kitangazwe lakini huku chini chini vitu vinafanyika wao wasie na wasi wasi tunafanya kazi,” amemaliza kwa kusema
Title:
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Mohammed Mpinga, amesema mara baada ya kusikia ajali iliyoua wanafunzi zaidi ya 30 wa S...
Post a Comment