Serikali mkoani Arusha imeahdi kuendelea kuboresha huduma za afya kwenye vituo vya afya ,pamoja na Zahanati mbalimbali zilizopo katika jiji la Arusha.
Hayo yamebainishwa na mkuu wa mkoa wa Arusha Bwana Mrisho Gambo katika muendelezo wa
ziara yake jijini Arusha alipokuwa anazindua nyumba ya mtumishi wa Afya
iliyojengwa na serikali katika zahanati ya NADOSOITO kata yaa Terati
jijini hapa.
Nyumba
hiyo iliyogarimu kiasi cha shilingi milioni 66.7 ambapo ni mradi
unatekelezwa kwa awamu wenye lengo la kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma za
afya katika jiji la Arusha kwa kuwaboreshea makazi watumishi waliopo
pembezoni.
Pamoja na hayo faida ya kukamilisha mradi huo umeongeza na kuboresha utoaji wa
huduma za afya katika jiji la Arusha hasa akina mama wajawazito na
watoto kutoka kata za Muriet,Terati,Daraja mbili na maeneo jirani.
Mradi
huo wa ujenzi wa nyumba ya mtumishi katika zahanati ya NADOSOITO
ulianza june 15 mwaka 2016 na utakamilika Mei 15, 2017 ambapo
mkandarasi kwa sasa anamalizia ujenzi wa nyumba hiyo kwa kuweka marumaru katika nyumba 2 na jiko la nyimbo hiyo.
Post a Comment