MOBISOL YAMPATA MSHINDI WA HAMASIKA NA MASIKA, AJINYAKULIA PESA TASLIMU
Kampuni ya Sola ya mobinsol nchini kupitia makao yake yaliyopo jijini Arusha,imetoa zawadi ya fedha taslimu laki mbili kwa mshindi wa kwanza wa droo ya kwanza ya hamasika na masika bwana Eliud Yona ambaye ni mkazi wa maji ya chai
Akitaja washindi wapili na mshindi wa tatu,Mratibu wa masoko Seth Mathemu alisema kwa tukio kama hili pia fanyika mkoa wa Singida ambako mshindi wa pili Ally Suwedi amekabidhiwa radio inayotumia sola ya mobisol huku mshindi wa tatu kutoka Kilindi kampeni akikabidhiwa mashine ya kunyolea
Mratibu ,alisema mashindano ya msimu wa Hamasika Masika ,umegawanyika droo tatu,ambako droo ya kwanza mshindi alipatikana tarehe 22 aprili, na mashindano ya droo ya tatu kuanza Mei mosi ,na droo ya mwisho kufanyika Juni moja
Alisema pia mshindi atapatikana kutokana na kasi ya kushawishi wateja kununua mitambo yao ya sola,ambako kwa droo ya tatu mshindi wa kwanza atapata fedha taslimu, huku mshindi wa pili na wa tatu kupata zawadi za bidhaa zao,na katika droo ya mwisho mshindi wa kwanza atajipatia zawadi ya bodaboda kutoka kampuni hiyo
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.