Mbunge wa Jimbo la Chalinze mkoani Pwani kwa tiketi ya Chama cha
Mapinduzi (CCM), Ridhiwani Kikwete amekanusha vikali shutuma
zilizotolewa dhidi yake kuhusu kujihusisha na biashara haramu ya dawa za
kulevya
Moja ya magazeti ya jana yalichapisha habari inayomtaja mbunge huyo
kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya ambayo imekuwa ikipigwa vita
kila kona ya nchi kutokana na kupoteza nguvu kazi ya taifa
Gazeti hilo limeandika kuwa jina la Ridhiwani limetajwa katika orodha ya
watuhumiwa wa dawa za kulevya na kuwa uchunguzi utafanyika. Pia
limesema mbunge huyo ametoa kauli nzito kwa hadhara
Kiongozi huyo kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema kuwa,'hafanyi
biashara hiyo haramu wala hakuwahi kufikiria kuifanya na kwamba nafsi
yake i tayari kufa masikini kuliko kupata utajiri kupitia njia hiyo
Aidha, ameeleza kuwa anaamini kwamba uchunguzi utafanywa ili kuweza
kuweka mambo sawa kwani yeye hana kitu chochote cha kuficha. Amesema
kwamba, maneno hayo ya shutuma juu yake ni uongo na kwamba yametolewa na
watu wasiomtakia mema na wasio na haya.
Post a Comment