Baada ya kukaa kituoni hapo kwa zaidi ya masaa mawili Waandishi wa habari waliokua nje ya eneo hilo walishuhudia Mwenyekiti huyo akichukuliwa na Gari aina ya Land Cruiser iliyofatwa na magari mengine nyuma yake na kuelekea ambako Waandishi hawakufahamu mara moja.
Baadaye msemaji wa CHADEMA Tumaini Makene alisema Polisi walienda na Mbowe kupekua nyumba zake na kuandikisha maelezo ya majirani ambapo alisema kwenye mida ya saa sita usiku wa kuamkia leo Polisi walimrudisha Mbowe kwenye kituo cha Polisi kati na wakamfungulia jalada la Uchunguzi….
Post a Comment