Askofu wa Kanisa Anglikana Dayosisi ya Dar es Salaam, Dk Valentino
Mokiwa amesema ataweka hadharani vitu anavyodai vitaonyesha ukweli wa
mgogoro uliopo katika dayosisi hiyo anayoiongoza.
Amesema baada ya siku saba, atawasilisha kwa waumini vitu vitakavyoeleza ukweli wa mambo kuhusu mgogoro unaondelea sasa.
Hivi karibuni, Askofu Mkuu wa kanisa hilo, Dk Jacob Chimeledya alimtaka
Mokiwa kujiuzulu kwa madai kwamba anatumia vibaya madaraka yake huku
akimtuhumu pia kwa ubadhirifu wa fedha.
Hata hivyo, Askofu Mokiwa alikana madai hayo na kusema mgogoro huo unatengenezwa na adui zake jambo linawavunja mioyo waumini.
Jana, akiweka jiwe la msingi la Kanisa la Kigango cha Mtakatifu Simon na
Yuda, lililopo Kimara Mavurunza ‘A’, Askofu Mokiwa alisema:
“Nipeni wiki hii inayoaanza kesho (leo), nikichelewa wiki moja na nusu
nitawaeleza ukweli; hakuna kitu kilichoibwa wala kukosewa, isipokuwa
waliokosea wanataka kutuvuruga.
Post a Comment