Pichani ni Katibu wa chama cha riadha mkoa wa Arusha Alfred Shahanga,ambaye pia ni muaandaaji wa Arusha Tourism Festival Picha na Vero Ignatus Blog. |
Baadhi ya wadau na washiriki katika mashindano katika tamasha la Arusha Tourism Marathon wakiwa wanafuatailia yanayoendelea uwanjani hapo.Picha na Vero Ignatus Blog |
Mshindi wa pili wa mbio za kilometa 5000 za
Atusha Tourism Marathon Gabriel Geay ametumia dakika
14:05:08.Picha na Vero Ignatus Blog
Wakwanza kutoka kulia ni mkurugenzi wa Arusha Media Musa Juma
akimnyanyua mkono mshindi wa Arusha Tourism Marathon Emmanuel Giniki
katikakatika mashindano hayo,Kutoka kulia ni Katibu wa chama cha
Riadha mkoani Arusha Alfredy Shahanga ,akifuatiwa na mshindi wa tatu
Ismail Juma ambaye alimaliza mbio hizo kwa kutumia dakika
14:11.60,akifuatiwa na mshindi wa pili Gabriel Geay .Picha na
Vero Ignatus BlogAfisa michezo Jiji la Arusha Benson Maneno wakwanza kushoto akijiandaa kuzindua mbio maalum za watoto wadogo walioshiriki katika Arusha Tourism Marathon akiwa pamoja na mwenyekiti wa Marathon mkoa wa Arusha |
Watoto wakiandwaliwa tayari kwa kukimbia mbio za mita
hamsini leo katika uwanja wa Shekh Amri Abeid,na wao wameshiriki
katika Arusha Tourism Marathon.Picha na Vero Ignatus
Blog.
|
Na.Vero Ignatus ,Arusha
Tamasha la Arusha tourism marathon limefanyika Leo jijini Arusha ikiwa ni awamu ya pili kufanyika mkoani haha ambapo mashindano hayo yameandaliwa na Arusha Media, Shahanga sport promotion Chini ya udhamini wa Tanapa.
Tamasha hilo limewashirikisha wanariadha kutoka mkoa wa Arusha, Manyara,pamoja na Kilimanjaro ambapo tamasha hilo likiwa limebeba kauli mbiu ya piga vita ujangili, tembelea Hifadhi zetu.
Mgeni rasmi katika tamasha hilo ni Afisa michezo wajiji la Arusha Benson Maneno ambapo amesema kuwa riadha imeutoa mkoa wa Arusha kimasomaso na Tanzania kwa ujumla michezo mingine bado imedorora
Amekipongeza chama cha riadha mkoa wa Arusha na kuwataka kuongeza juhudi zaidi kwani michezo ni ajira,hujenga mwili kiafaya ,pia michezo humtambulisha mtu kitaifa na kimataifa pia, amewataka vijana kuchangamkia fursa hayo.
Katibu wa riadha mkoa wa Arusha kuwa Alfred Shahanga ambapo pia ni muandaaji mwenza wa Arusha Tourism Festival amesema kuwa mashindano hayo yalianza mwaka 2015 walianza na mbio za barabarani huku safari hii wameamua kurudi uwanjani ili kuhamasisha mbio fupifupi ambazo kuwamuda mrefu zimesahaulika.
"Mashindano haya kwetu sisi yameonyesha ufanisi mkubwa kwani mshindi wa kwanza katika mbio za mita 5000 ameweka rekodi ya uwanja namaanisha muda aliokimbia ni rekodi ya uwanja huu."alisema Shahanga.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Arusha Media Mussa Juma amesema kuwa lengo kubwa la mashindano hayo ni kuhamasisha michezo katika mkoa wa Arusha pamoja na kuutangaza Utalii wa ndani
"Tumewashirikisha watoto wadogo katika mashindano haya kwani hawa nimabalozi wabaadae ambao watakuja kupiga vita ujangili,watawahamasisha kizazi kijacho michezo , na watautangaza vyema utalii wandani hapo badge."alisema Mussa.
Mashindano hayo yameambatana na utoaji wa zawadi kwawashindi ambapo wasindi wa mbio za kilometa 3000 kwaupande wanawake mshindi wa kwanza alipewa zawadi ya shilingi 150,000 na wale wa mbio za kilomita 5000 mshindi wakwanza amepatiwa zawadi ya shilingi 200,000.
Post a Comment