Tuzo
aliyotunukiwa mkurugenzi mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei
siku ya Alhamisi Septemba 22, 2016 jijini New York nchini Marekani
katika hotel ya St. Regis, New York. African Leadership hutoa tuzo
katika kutambua michango unaotolewa na viongozi wa bara la Afrika katika
kuleta maendeleo na utendaji wa kazi wenye ufanisi' katika kukuza
uchumi kwa kusaidia kukuza na kuwainua wawekezaji wazawa. African
Leadership ilishawahi kutoa tuzo kama hilo kwa Rais mstaafu Jakaya
Kikwete mwaka April 9, 2014 katika hotel ya St Regis ya Washington, DC.
Picha na Vijimambo Blog/Kwanza Production, New York.
Mkurugenzi
Mtendaji wa benki ya CRDB, Dkt Charles Kimei akifuatilia hafla ya
utoaji tuzo kwa viongozi wa Afrika iliyofanyika siku ya Alhamisi Sepemba
22, 2016 katika hotel ya St. Regis New York. Kulia ni Rais wa Burkina
Faso, Mhe. Roch Marc Christian Kabore.
kushoto ni Mkurugenzi wa masoko, utafiti na huduma kwa wateja, Bi. Tully Esther Mwambapa akisalimiana na Rais wa Malawi Mhe. Prof. Arthur Peter Mutharika mara tu baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dkt Charles Kimei kupokea tuzo iliyotolewa na African Leadership siku ya Alhamisi Septemba 22, 2016 katika hotel ya St. Regis, New York. kulia ni fisrt lady Mke wa Rais wa malawi.
Picha ya pamoja.
Kutoka
kushoto ni Mkurugenzi wa fedha wa benki ya CRDB, Bwn. Frederick
Nshekanabo, Mkurugenzi wa masoko, utafiti na huduma kwa wateja, Bi.
Tully Esther Mwambapa wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dkt Charles Kimei alipokua
akifanyiwa mahaojiano mara tu baada ya kupokea tuzo kutoka African
Leadership katika hotel ya St. Regis, New York siku ya Alhamisi Septemba
22, 2016.
Mkurugenzi
wa masoko, utafiti na huduma kwa wateja, Bi. Tully Esther Mwambapa
akifuatilia sherehe ya Tuzo kutoka kwa African Leadership iliyofanyika
katika hotel ya St. Regis, New York siku ya Alhamisi Septemba 22, 2016. Kulia ni Rais wa Burkina Faso, Mhe. Roch Marc Christian Kabore.
Hapa
ni siku Balozi wa Nigeria nchini Marekani Profesa Adebowele Adufye,
alipomkabidhi aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Mheshimiwa Bernard Membe Tuzo la Kiongozi Mwenye Mchango
Mkubwa Zaidi Katika Maendeleo ya Bara la Afrika kwa mwaka 2013
anayopokea kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya
nne Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete wakati huo katika sherehe ya
kutunuku Tuzo hiyo kwenye Hoteli ya St. Regis mjini Washington, D.C.,
usiku wa , Jumatano, Aprili 9, 2014
Post a Comment