Watoto wakishandana kukimbia na yai
katika siku ya mtoto wa Africa iliyoandaliwa na bank ya CRDB tawi la Usa River
wilaya ya Arumeru mkoania Arusha katika viwanja vya usa river academy.
|
Watoto wakishandana kukimbia katika siku ya mtoto wa Africa iliyoandaliwa na bank ya CRDB tawi la Usa River wilaya ya Arumeru mkoania Arusha katika viwanja vya usa river academy. |
Watoto wakishandana kukimbia na yai
katika siku ya mtoto wa Africa iliyoandaliwa na bank ya CRDB tawi la Usa River
wilaya ya Arumeru mkoania Arusha katika viwanja vya usa river academy.
|
Watoto wakishandana kukimbia na magunia katika siku ya mtoto wa Africa iliyoandaliwa na bank ya CRDB tawi la Usa River wilaya ya Arumeru mkoania Arusha katika viwanja vya usa river academy |
Na Ferdinand Shayo,Arusha
Benki ya CRDB tawi la Usariver
imewahimiza wazazi na walezi kujenga
tabia ya kuwaendeleza watoto katika
michezo na vipaji walivyonavyo ili viweze kuwaimarisha kiakili na kimwili na
kuwanufaisha baadae.
Meneja wa Tawi hilo Jenipher
Tondi ameyasema hayo katika michezo ya watoto iliyoandaliwa na benki hiyo
katika viwanja vya USARIVER ACADEMY ambapo watoto walipata fursa ya kucheza
michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu,netiboli,kukimbiza kuku na mbio za
kukimbiza magunia..
Amesema kuwa wazazi hawana budi
kuendeleza vipaji vya watoto kwani vinaweza kuwa na faida kwa familia,jamii na
taifa. “wazazi wawape watoto nafasi ya kushiriki katika michezo ili kuweza
kuvumbua vipaji vyao vilivyojificha sababu vipaji ni ajira tosha”
Pia amewakumbusha wazazi kuwawekea
watoto akiba ya fedha kwa ajili ya kumsaidia mtoto katika kulipa fedha za ada
kwa kufungulia account zisiszo kuwa na riba.
Kwa upande wao watoto walioshiriki
katika michezo hiyo Oscar Damian na Angela John wameishukuru benki hiyo kwa
kuwajali na kuwapa nafasi ya kukutana na watoto wenzao ambapo wameweza
kuburudika na michezo iliyoandaliwa.
Jane Nassari amewataka wazazi
kujenga utamaduni wa kuwaruhusu watoto wao kushiriki kwenye michezo kwasababu
michezo huleta afya ya akili,furaha na mashirikiano.
Post a Comment